Ushirika wa Imani
> Juma 5 > Dokezo
 |
|
Dokezo:
Habari! Karibu mara ya mwisho kwenye Nyenzo yetu ya Usalama ya FAST. Ni ombi letu kwamba mpango huu umekuwa baraka kwako—ukikupa zana zenye manufaa ili kuwa salama kama Mkristo.
Kanuni hizi ni muhimu sana, ni wazo zuri kujikumbusha mara kwa mara. Kila baada ya miezi michache yapitie tena masomo hayo. Au bora zaidi, mtafute rafiki fulani, na kumjulisha kuhusu kozi hii. Kuna mengi zaidi kwa ajili ya maisha ya Kikristo, lakini hatupaswi kamwe kupoteza mtazamo wa mambo ya msingi!
Na ni tumaini letu, kufikia sasa, unaanza kuona kukariri Maandiko kama moja ya misingi hiyo. Tena na tena Mungu anawaagiza watoto Wake walihifadhi Neno mioyoni mwao: Kumbukumbu la Torati 6:6, I Wakorintho 15:1-2, Ayubu 22:22, Mithali 7:1-3, Wakolosai 3:16, nk.
Lakini Mungu anafanya zaidi ya kutuamuru tu kukariri—Yeye hulibariki Neno Lake, na kulifanya liwe baraka maishani mwetu. Biblia inakuwa tamu sana kiasi kwamba hatuwezi kamwe kufikiria kuiacha! Rafiki, songa mbele. Pata ladha nzuri wewe mwenyewe.
Mhariri,
Amefichwa katika Kristo |
These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST
Ushirika wa Imani
Survival Kit > Juma 5 > Malengo
 |
Karibu katika Uchunguzi wetu wa tano na wa mwisho wa Biblia. Somo hili linazungumzia moja ya dondoo muhimu zaidi katika mafanikio ya maisha ya Kikristo. Tunaiita Ushirika wa Imani. Ili kuiweka kirahisi, tunahitajiana sisi kwa sisi. Ikiwa tunakusudia kwa dhati kusonga mbele—lazima tuwe makini kuhusu kusonga mbele pamoja! |
 |
Aya yako ya tano ya kukariri ni ndefu kidogo kuliko zingine, lakini ni nzuri: Waebrania 10:24-25. Anza kuifanyia kazi mapema katika juma. Pia, hakikisha umemudu vilivyo aya zako nne zingine. Rudia, rudia, rudia! Hebu fikiria, hivi karibuni utajua aya zako “kadhaa” kamili za kwanza! Hata hivyo, usiishie tano—kuna mengi zaidi zilikotokea hizo! |
 |
Dondoo zako mbili za mwisho za kukariri ziko hapa tu mbeleni. Soma kwa makini Mapendekezo Kutendea Kazi, kisha yarudie pamoja na dondoo zingine nane ambazo umejifunza hadi sasa—mpaka uweze kukariri zote kumi kwa mpangilio. Pia, tumia muda kidogo kufikiria mipango yako ya kuendelea zaidi kulikariri Neno. Je, umeamua kwa dhati kudumu kufanya hivyo? Tunatumaini hivyo! |
Hata milele sitayasahau maagizo Yako:
Maana kwa hayo umenihuisha.
Zaburi 119:93
Ushirika wa Imani
Survival Kit > Juma 5 > Uchunguzi wa Biblia
Karibu kwa Uchunguzi wa Biblia wa mwisho katika mpango wetu wa Nyenzo za Usalama. Somo hili linashughulikia dondoo moja muhimu zaidi katika usalama: ushirika unaojengwa kwenye Biblia. Mungu hakukusudia yeyote miongoni mwetu aipitie njia ya Kikristo peke yake. Badala yake, mpango Wake ni sisi kufurahia mahusiano maridhawa ya kiroho. Hakikisha kuungana na waumini wenzako daima kunabaki kuwa sehemu muhimu ya maisha yako!
Hebu tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. Waebrania 10:24-25
1. |
Nini kusudi halisi la ushirika wa Kikristo? Waebrania 10:24-25
Kumbuka: Mungu anajua tunahitaji kutiwa moyo na kuhimizwa na Wakristo wengine ili kufanikiwa katika maisha ya Kikristo. Hitaji hili litazidi tu kuongezeka kadiri tunavyoukaribia zaidi na zaidi ujio wa pili wa Yesu Kristo.
|
2. |
Kwa nini aina hii ya ushirika ni muhimu sana? Waebrania 3:13-14
Kumbuka: Ni hatari kujaribu na kusalimika kama Mkristo kwa uwezo wetu wenyewe. Fanya kila liwezekanalo ili kupata ushirika wa Kikristo unaokuza imani na kisha jipatie faraja na mausia unayohitaji!
|
3. |
Je, nini kusudi la mausia? Waefeso 4:15
Kumbuka: Mausia kimsingi ni kusema yale mambo yatakayomsaidia mtu mwingine kufanana zaidi na Yesu. Ili kuwa na ufanisi zaidi, yanapaswa daima kutoka kwenye moyo wa upendo.
|
4. |
Nini kinapaswa kuwa kifungo kinachowaunganisha waumini pamoja katika ushirika? Wakolosai 3:14
Je, hii inatoka wapi? Warumi 5:5
|
5. |
Soma 1 Wathesalonike 2:7-13. Zipi baadhi ya njia ambazo kwazo upendo wa Paulo kwa ajili ya waumini hawa zinaweza kuonekana?
|
6. |
Kwa jinsi gani upendo wa Paulo ni dhahiri katika 1 Wathesalonike 3:5-11?
|
7. |
Tathimini maisha yako. Kwa namna gani upendo wako kwa ajili ya ndugu na dada zako katika Kristo unalingana na ule wa mtume Paulo?
Kumbuka: Ushirika halisi ni fursa ya thamani! Lakini hautokei kwa bahati nasibu—unahitaji kazi, azma, na jitihada ili kupata na kujenga mahusiano imara. Ndiyo, urafiki huchukua muda, lakini thawabu husika inawiana nayo.
|
8. |
Paulo alisema nini kingekuwa matokeo ya mwisho ya kujifunza kupendana sisi kwa sisi? I Wathesalonike 3:12-13
Kumbuka: Ajabu! Paulo alikuwa na shauku ya kuona mioyo ya waumini hawa wapya ikiwa imeimarishwa katika utakatifu—na alishawishika kwamba upendano wa mshiriki na mshiriki ndio ambao ungetimiza hilo!
|
9. |
Soma Mathayo 22:36-39. Je, nuru gani ambayo aya hizi huangaza kuhusu umuhimu wa ushirika wa Kikristo?
Kumbuka: Ushirika wa Kikristo husimama kwenye makutano ya amri kuu mbili za Biblia: upendo kwa mtu na mwenzake unaojengwa katika upendo wao kwa Mungu. Nini kingeweza kuwa muhimu zaidi ya hilo?
|
10. |
Je, una mipango gani ya kuhakikisha unapokea baraka za ushirika endelevu wa Kikristo katika siku zijazo?
|
Sasa umekamilisha Uchunguzi wa mwisho wa Biblia katika Nyenzo yetu ya Usalama ya FAST. Umechunguza ukweli uletao furaha kwamba Mungu ana mpango maridhawa kwa ajili ya maisha yako, nguvu ibadilishayo ya akili iliyojikita katika Kristo, siri ya kuinuka tena unapojikwaa dhambini, jinsi ya kutambua mwelekeo wa Mungu unapotatanika, na baraka za ushirika halisi wa Kikristo. Yote ni muhimu sana ikiwa unataka kusalimika—na kustawi—katika mwenendo wako wa Kikristo. Je, uko tayari kuazimu hivi sasa ili kujenga kanuni hizi tano za msingi maishani mwako?
 |
Ndiyo |
|
 |
Hapana |
Ushirika wa Imani
Survival Kit > Juma 5 > Mapendekezo Kutendea Kazi
Karibu kwenye dondoo zetu mbili za mwisho za kukariri. Je, zimesaidia hadi sasa? Je, umefanikiwa kujifunza aya zako? Je, unaweza kuzinukuu kila neno kamilifu? Je, unajua marejeo yao? Je, unatafakari juu ya aya zako, na kuzitumia maishani mwako? Marudio yako kila siku yakoje? Juma hili tutaangalia dondoo mbili zaidi za kukariri Maandiko—dondoo zitakazokusaidia kuendelea kukariri kwa uaminifu katika majuma na miezi ijayo. Jifunze kwa maombi!
Dondoo #9. Panga Hatua.
Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno Langu, mmekuwa wanafunzi Wangu kwelikweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. Yohana 8:31-32
Muhimu zaidi kuliko jinsi ulivyodhamiria kukariri sasa hivi—ni jinsi utakavyodumu kwa uthabiti barabarani. Je, bado utakuwa ukiendelea kukariri miaka mitano kuanzia sasa? Kwa miezi mitano? au hata katika majuma tano? Aya mbili kwa juma zitakuwa elfu moja kwa miaka kumi, lakini ikiwa tu utadumu kwa uthabiti—kwa miaka kumi!
Unadumuje kuwa thabiti? Hili tu: panga hatua. Anza kwa aya moja au mbili kwa juma. Hilo likiwa rahisi sana, jaribu kujiwekea lengo la aya tatu au nne kwa juma. Jambo la msingi ni kuweka kanuni ya kutokariri KAMWE chini ya lengo lako. Unaweza kukariri zaidi wakati wote—lakini hupaswi kuruhusu juma moja lipite unapokariri pungufu. Hatuzungumzii idadi yako ya aya
kwa wastani. Tunazungumzia lengo la chini unalotimiza kila wakati...
Iwapo unahitaji msaada wa kuchagua aya ili kujifunza, tuna nyenzo madhubuti kwa ajili yako kwenye programu ya FAST. Tunakiita Kikaririshi cha Dakika, na kina aya 52 makini za kuanzia unazoweza kujifunza kwa dakika moja au chini ya hapo. Hiyo ni aya moja kwa juma kwa mwaka! Ili kujitwalia, nenda kwenye: WWW.FAST.ST/MINMEM. Ifikirie kama zawadi yetu ya bure kwako kwa ajili ya kufika hadi mwisho wa masomo haya!
Pia tuna kozi nyingi zaidi za mwongozo wa kujifunza kama huu, pamoja na aya zaidi zilizopendekezwa. Kozi hizi ni njia nyingine bora ya kukusaidia kusonga mbele katika kukariri kwako.
Dondoo #10. Wajibika Kiasi Fulani.
Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. Maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu hadi mwisho. Waebrania 3:13-14
Moja ya dondoo kuu za mafanikio katika kukariri Maandiko, ni uwajibikaji wa muda mrefu. Usithubutu kulifanya peke yako! Bila uwajibikaji, ni rahisi sana kulegea—kwanza juma moja, na kisha lingine. Punde programu yako yote ya kukariri Maandiko imeharibika!
Ili kuepuka hili, jaribu kumtafuta rafiki mmoja au wawili walio tayari kukutana nawe kila juma, na kukukagulia aya zako mpya. Hata jambo bora zaidi, mtafute mtu fulani mwenye shauku ya kukariri kando yako, na ukague aya zake pia. Unaweza pia kupenda kuwa sehemu ya Klabu ya Kukariri isiyolipishwa, mtandaoni kwenye programu ya FAST.
FAST, kama ambavyo pengine unajua, ni jumuia ya mtandaoni, yenye maelfu ya wanachama duniani kote. Na Klabu yetu ya Kukariri ni njia bora ya kupanua mduara wako mahalia wa usaidizi. Tunaendelea daima kuwasilisha nyenzo mpya katika jumuia yetu, na tungependa ujiunge. Ili kufanya hivyo, tembelea tu
WWW.FAST.ST/CLUB.
Wakati fulani unaweza hata kutaka kufikiria kuunda kikundi kidogo kanisani mwako, na kuwaongoza kupitia Nyenzo ya Usalama—na kisha pengine baadhi ya kozi zetu za juu zaidi za mafunzo. Kuwafundisha wengine kanuni ambazo umejifunza ni njia makini ya kuziimarisha zaidi akilini mwako. Kwa maelezo kuhusu jinsi ya kuongoza timu ya FAST, tafadhali angalia Mwongozo wetu wa Viongozi bila malipo katika
WWW.FAST.ST/LM.
Mpango wa Mungu kwako ni kuliandika Neno Lake moyoni na akilini mwako. Naye anatamani kufanya hivyo. Ni ombi letu kwamba masomo haya yamekupa zana na mafunzo unayohitaji ili kushirikiana Naye!
Je, uko tayari kuchukua hatua inayofuata? Tafuta kozi yetu ya Mafunzo ya Msingi, hatua inayofuata katika Njia yetu ya Uanafunzi. Gundua dondoo madhubuti za kivitendo kwa ajili ya stadi za kimsingi za uanafunzi, na uimarishe kutembea kwako na Mungu. Maisha yako hayawezi kuwa vilevile tena!