Njia Iliyo Mbeleni
Survival Kit > Juma 4 > Dokezo
 |
|
Dokezo:
Habari! Karibu tena mara nyingine. Ni ombi letu kwamba programu hii inathibitisha kuwa baraka kwako—ikikupa maarifa maridhawa kuhusu jinsi unavyoweza siyo tu kusalimika kama Mkristo, bali pia kustawi. Somo hili linaangalia eneo lingine muhimu: jinsi ya kutambua mwelekeo wa Mungu kwa ajili ya maisha yako. Ikiwa umewahi kujiuliza jinsi ya kujua mapenzi ya Mungu, majibu yako mbele kidogo tu!
Na ingawa hatujui mipango kamili ya Mungu kwa ajili ya maisha yako, tunafahamu hili: hakuna ukomo wa kile ambacho Mungu anaweza kufanya kwa mtu mmoja atakayejikabidhi kikamilifu kwa Kristo na kumpa Roho Wake nafasi ili atende kazi moyoni mwake. Hakuna ukomo!
Tunajua hili pia: kwamba mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yako umeandikwa katika Neno Lake. Maelekezo yote unayohitaji yapo hapo, yakikungoja wewe tu uchimbe na kuyapata. Utapata ahadi za kudai, ushauri wa kufuata, na maonyo ya kuzingatia. Na yamejaa mawazo bora!
Ndiyo, yote yamo humo—kwenye Neno. Kwa hivyo fanya kinachowezekana ili kuweka kiasi kikubwa cha Neno hilo moyoni mwako kadiri uwezavyo!
Mhariri,
Amefichwa katika Kristo |
These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST
Njia Iliyo Mbeleni
Survival Kit > Juma 4 > Malengo
 |
Uchunguzi Wako wa Biblia juma hili ni jambo lingine muhimu. Unaitwa Njia Iliyo Mbeleni, na hutazama jinsi ya kutambua uongozi wa Mungu maishani mwako. Mungu ana mipango mikubwa kwa ajili ya kila mmoja wetu, lakini lazima tujifunze kuuafiki uongozi Wake ili mipango Yake itimie kikamilifu. Tunaomba somo hili lisaidie. |
 |
Je, uko tayari kwa ajili ya aya yako inayofuata? Je, umejifunza vizuri zile zako tatu za kwanza? Kumbuka, unapaswa kuendelea kujikumbusha kila moja ya aya hizi angalau mara moja kwa siku. Hakikisha unazitunza katika moja ya mifuko ya ndani ya kifurushi chako cha aya. Inapaswa kuchukua dakika moja au mbili tu kujikumbusha. Aya yako juma hili ni ile inayopendwa na wengi: Mithali 3:5-6. |
 |
Umefikia dondoo ya kumbukumbu ya saba na nane! Je, unaweza kukariri zile sita za kwanza? Jambo muhimu zaidi, hivi unazitumia katika jitihada zako za kulihifadhi Neno la Mungu moyoni mwako? Dondoo mbili zinazofuata ni muhimu kama zile zingine, kwa hiyo soma kwa makini Mapendekezo Kutendea Kazi ya juma hili. Jaribu kuandika kutoka akilini dondoo zote ambazo tumejifunza hadi sasa angalau mara moja juma hili—kwa mpangilio. Je, unaweza kulifanya hilo? |
Ulimi wangu utanena ahadi Yako:
Maana maagizo Yako yote ni ya haki.
Zaburi 119:172
Njia Iliyo Mbeleni
Survival Kit > Juma 4 > Uchunguzi wa Biblia
Karibu tena kwenye somo lingine katika usalama wa Mkristo. Uchunguzi huu wa Biblia unaangalia jinsi Mungu anavyoongoza na kuelekeza katika maisha ya Mkristo. Mara nyingi maamuzi madogo tunayofanya yana matokeo ya kudumu—na zaidi sana yale makubwa! Inatia moyo jinsi gani basi, kumjua kwamba Mungu yuko tayari kutuongoza katika hayo yote.
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote; wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri Yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Mithali 3:5-6
1. |
Je, ni fursa gani moja ya kuwa mwana wa Mungu? Warumi 8:14
Kumbuka: Maisha yamejaa fadhaa na dhiki. Hata hivyo, Mungu asifiwe, yuko tayari kutuongoza kama wana na mabinti wake.
|
2. |
Jinsi gani ungeweza kuandika muhtasari kuhusu shauku ya Mungu kwa ajili ya kila mmoja wetu? Wakolosai 1:9
Kumbuka: Kujazwa maarifa ya kuyajua mapenzi ya Mungu ni kujazwa maarifa ya Neno Lake—maana mapenzi ya Mungu yanapatikana katika Biblia. Hii ndiyo sababu mojawapo kumbukumbu ya Maandiko ni muhimu sana!
|
3. |
Ipi njia ni ya msingi ambayo Mungu hutafuta kutuelekeza?
Zaburi 119:33-35
Zaburi 119:59-60
Zaburi 119:97-100
Zaburi 119:116-117
Zaburi 119:133
Kumbuka: Mausia ya Mungu kuhusu mada yoyote yanaweza kuchunguzwa katika Maandiko. Ukitafuta utapata.
|
4. |
Roho hutuongozaje mara nyingi?
Isaya 30:21
Yohana 14:26
Kumbuka: Mara nyingi Mungu hurejesha akilini mwetu aya fulani za Maandiko ambazo tumekariri katika hali maalumu kwa wakati ufaao, ili kutupatia mwongozo kamili tunaohitaji.
|
5. |
Je, Mungu anataka kutuelekeza vyema kiasi gani katika kila moja ya maeneo yafuatayo?
Matendo: I Wakorintho 10:31
Maneno: Waefeso 4:29
Mawazo: Wafilipi 4:8
Kumbuka: Mungu anajihusisha kwa dhati na mafanikio yetu kiasi kwamba yuko tayari kutupatia mwelekeo hata katika mambo madogo kabisa maishani. Kwa mwongozo kama huo, nani awezaye kushindwa?
|
6. |
Nini ambacho wakati fulani kinahitajika ili kutambua maelekezo ya Mungu kupitia neno?
Maombolezo 3:25
Hosea 12:6Therefore turn thou to thy God: keep mercy and judgment and wait on thy God continually.
Mika 7:7
Kumbuka: Kama unakabiliwa na uamuzi mgumu, hakikisha unatumia muda wa ziada kumtafuta Mungu kupitia Neno na umngojee azungumze. Iwapo ni lazima ufanye uamuzi—fanya lililo bora kadiri uwezavyo, kwa kuzingatia kanuni ambazo Mungu amekupa kupitia Neno Lake hadi hatua hiyo.
|
7. |
Je, tunapaswa kufanya nini wakati “hisia” zetu zinapoonekana kupingana na Neno?
Isaya 8:20
Mithali 19:21
Zingatia: Ukihisi unaelekezwa kufanya jambo ambalo linakiuka kanuni ya Neno la Mungu, tambua hakika kwamba si Mungu!
|
8. |
Kutakuwa na matokeo gani ya kumruhusu Mungu aongoze maishani mwetu? Kumbukumbu la Torati 28:1-2
|
Ni wazo la pekee ajabu ilioje—hekima ya Mwenyezi Mungu inapatikana kwetu! Yule ajuaye mawazo na nia ya kila moyo, na aionaye kesho kwa uwazi kama ilivyo leo, yuko radhi kuongoza hatua zetu katika kila shaka na jaribu. Zaidi ya hayo, upendo Wake mkuu kwetu na shauku Yake juu ya mafanikio yetu, hutupatia hakikisho kwamba uongozi Wake daima ni kwa ajili ya manufaa yetu bora. Vipi kuhusu wewe? Je, uko tayari kutafuta mwongozo wa Bwana kwa ajili ya maisha yako? Kuchunguza Maandiko na kisha kufuata mapenzi Yake yaliyofunuliwa? Hakuna kitabu bora cha mwongozo zaidi ya hiki!
 |
Ndiyo |
|
 |
Hapana |
Njia Iliyo Mbeleni
Survival Kit > Juma 4 > Mapendekezo Kutendea Kazi
Watu wengi, wanapoanza kufahamu jinsi ambavyo dondoo za kumbukumbu ambazo wamekuwa wakijifunza zilivyo madhubuti hasa, husisimka sana kuhusu kukariri, kiasi kwamba hufanya kosa kubwa. Wanaanza kujaribu kukariri kupita kiasi—pengine wanaamua kukariri orodha ndefu ya aya zinazohusu mada mahususi. Au wanajaribu kujifunza sura nzima, au hata vitabu vizima vya Biblia. Ingawa hizi ni juhudi bora, kinachotokea kwa kawaida ni kwamba mambo punde hugeuka kuwa kukariri kimazoea—na kuna matokeo kidogo au hakuna kabisa maishani. Tunapendekeza badala yake ujikite kwenye aya zinazofungamana kwa ukaribu na mwenendo wako binafsi na Mungu. Hiki hapa ndicho tunamaanisha:
Dondoo #7. Kariri Aya Unazofahamu.
Na maneno haya, ninayokuamuru leo, yatakuwa moyoni mwako. Kumbukumbu la Torati 6:6
Kwanza, mwombe Mungu aanze kukuonesha aya mahususi anazotaka ukariri. Ikiwa unatumia muda pamoja na Mungu kila asubuhi, katika maombi na kujifunza Biblia, pengine tayari ameanza kugusia aya fulani muhimu moyoni mwako. Labda umeanza kuona aya unazosikia katika mahubiri, au labda rafiki fulani ana kipaji cha kuwasilisha Maandiko hususan yenye kutia moyo. Labda umekutana na aya ya kuvutia katika masomo haya ya Nyenzo za Usalama. Hata hivyo Mungu hukutumia aya—tunapendekeza uzikariri zikingali mawazoni. Ikiwezekana, siku hiyo hiyo!
Mungu anapozungumza na mioyo yetu, anasema jambo analotaka tukumbuke. Na anatutaka tupitie masomo hayo, tena na tena, ili kuhakikisha yanaleta matokeo ya kudumu maishani mwetu. Kwa hiyo hatutasahau yale ambayo ametufundisha. Tazama Kumbukumbu la Torati 4:9. Badala ya kupanga aya zipi ukariri, jifunze kusikiliza, na mruhusu Mungu aongoze.
Aya zilizopangwa ni nzuri—hasa wakati wa kuanza, lakini zinapaswa kujalizwa kwa aya ulizopewa moja kwa moja na Mungu. Na hatimaye utataka kutengeneza aya muhimu unazogundua peke yako, asilimia kubwa na kubwa zaidi ya aya unazojifunza. Ni aya hizi za hivi karibuni na binafsi ambazo zitakuwa na maana zaidi maishani mwako. Kwa hiyo uwe macho. Na jifunze kuzitafuta asubuhi baada ya asubuhi kadiri unavyokutana na Bwana.
Dondoo #8. Jikite katika Vifungu Vifupi.
Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini? Maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo. Isaya 28:9-10
Ingawa inashawishi, epuka kujaribu kukariri vifungu virefu, kama vile sura au vitabu vizima vya Biblia—hasa mwanzoni. Anza na aya moja au mbili tu, hapa na pale. Hivi ndivyo Roho Mtakatifu anavyofundisha—amri juu ya amri, mstari juu ya mstari, “akilinganisha mambo ya kiroho na ya kiroho” (1 Wakorintho 2:13). Huhitaji kukariri kifungu chote ili kuelewa muktadha wa aya moja—na kamwe si lazima sana kunukuu sura nzima ili kujibu swali au pingamizi la rafiki fulani. Badala yake jikite kukariri aya muhimu na kisha jumuisha aya hizo maishani mwako. Vifungu virefu siyo tu kwamba vina changamoto zaidi kukariri, lakini pia ni vigumu zaidi kujikumbusha, na ni vigumu zaidi kuvihifadhi.
Kwa kweli, zinaweza kuwepo nyakati unazoweza kutaka kujaribu kile ninachoita kupunguza aya. Yaani, badala ya kukariri, aya ndefu mgumu, zingatia kukariri sehemu ile tu ya aya ambayo Mungu anakugusa ujifunze. Aya kama Esta 4:14, na Zekaria 4:6, ni ndefu na ngumu kujifunza—lakini kuna sehemu nzuri katika aya hizo ambazo ni rahisi sana kujifunza na zenye nguvu sana. Maandiko yote ni muhimu, lakini hakuna chochote kilichovuviwa kuhusu migawanyo yetu ya kisasa ya sura na aya—kwa hiyo jisikie huru kuchagua migawanyo yako mwenyewe kadiri Mungu anavyokuongoza. Utakusanya aya nyingi zaidi, kwa haraka zaidi.
Unaweza kuzirudia wakati wowote baadaye, bila shaka, na kukariri sehemu iliyosalia ya aya fulani ambayo umeipunguza, au hata kujaribu kifungu kirefu ukipenda. Kuhusu kifungu fulani, chagua kimoja chenye sehemu kadhaa ambazo tayari unajua na ujaze tu vipande vilivyokosekana, aya moja au mbili kwa wakati. Na hakikisha unafuata kanuni zote ambazo tumezungumzia hadi sasa kadiri unavyofanya—kwa kila aya moja. Weka kipaumbele maalumu kwenye kila rejeleo binafsi.
Lakini tena, kuwa makini. Epuka kujaribu vifungu virefu zaidi hadi pale ambapo kukariri Biblia kumekuwa mwenendo wa maisha, na unapokuwa umefanikisha mamia kadhaa ya aya ili kuthibitisha hilo! Uvumilivu wako utatunukiwa.