Kukabili Jaribu

Survival Kit > Juma 3 > Dokezo

     

Dokezo:


Unaendeleaje hadi sasa? Je, umekuwa ukiupa mpango huu juhudi zako bora zaidi? Je, unakariri aya zako? Je, unakamilisha hatua yako ya Kuichunguza Biblia? Je, unajifunza dondoo zako za kumbukumbu? Muhimu zaidi, je, unatekeleza yale unayojifunza? Masomo haya yanashughulikia mada muhimu sana. Jipatie kila kitu kutoka kwayo kadiri unavyoweza.

Wakati fulani Yesu alitumia mfano wa kuvutia ili kueleza umuhimu wa kulihifadhi Neno la Mungu moyoni. “Ufalme wa mbinguni,” alisema, “umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote” (Mathayo 13:33).

Unaona, mara unapoanza kulihifadhi Neno moyoni mwako, linaanza kufanya kazi—kidogo kidogo—hadi maisha yote yanabadilishwa. Haitokei mara moja, lakini huanza mara moja! Kwa hiyo ingia katika Neno. Songa mbele katika hatua yako ya kuikariri Biblia. Jipatie chachu yote ya kiroho kadiri uwezayo!

Mhariri,
Amefichwa katika Kristo

These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST

Kukabili Jaribu

Survival Kit > Juma 3 > Malengo


Jina:                                                     Saini:                                         
Tarehe:                                         


Natumai unafurahia hatua yako ya Kuichunguza Biblia. Somo la juma hili linaitwa Kukabili Majaribu, na linaangalia tatizo la dhambi. Majaribu hutujia kila mmoja wetu—basi ni muhimu ilioje kwamba tujifunze kuyashughulikia kisahihi! “Kabili” somo hili kwa maombi.

Aya ya kukariri juma hili inapendwa na wengi: I Yohana 1:9. Tumia muda fulani kuitafakari. Je, inaahidi baraka gani mbili? Masharti ni yapi? Inasema nini kuhusu tabia ya Mungu? Tumia ujuzi wako wa kutafakari ili kupata vidokezo vyote katika aya hii kadiri uwezavyo. Rudia aya zako zingine kila siku hadi uweze kunukuu zote tatu kwa usahihi.

Dondoo zako za kumbukumbu zinazofuata zinajadili jinsi ya kuhamisha aya kutoka kwenye kumbukumbu yako ya muda mfupi hadi kumbukumbu yako ya muda mrefu. Hebu fikiria—siyo tu kuweza kukariri aya fulani, lakini kuweza kuihifadhi! Pia utagundua jinsi ya kukumbuka marejeleo. Siyo ngumu: soma tu Mapendekezo Kutendea Kazi ya juma hili na ufuatilie kwa kina. Endelea kurudia rudia dondoo zote sita kila siku. (Unaweza kuamua kuziandika kwenye kadi ya aya na kutunza orodha husika katika furushi la aya). Dondoo nne zaidi zimesalia!


Kwa mausia Yako najipatia ufahamu:
Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
Zaburi 119:104


Kukabili Jaribu

Survival Kit > Juma 3 > Uchunguzi wa Biblia

Ingawa Mungu ana mpango mkuu kwa ajili ya maisha yetu (Uchunguzi wa Kwanza wa Biblia), na utajiri wote wa mbinguni unapatikana kwetu kupitia Kristo (Uchunguzi wa Biblia wa Pili), wakati mwingine tunajikwaa. Majaribu yananyemelea na kuingia, dhambi inatushinda, hatia inatulemea. Kwa bahati nzuri, Mungu amefanya mpango kwa ajili ya vipindi kama hivyo hasa, na kuuelewa mpango huo ni muhimu sana—ili kuokoka kwetu.

Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote. I Yohana 1:9


1.

Ni tatizo gani moja ambalo Biblia inaeleza kwamba linawakabili wote? I Wakorintho 10:13






Kumbuka: Jaribu letu kuu ni kuruhusu mambo ya ulimwengu huu kutukengeusha tuache kumtazama Kristo.
   

2.

Nini chanzo cha tatizo hili? Yakobo 1:13-15







Kumbuka: Tangu wakati wa kuzaliwa, tumefungiwa katika vita vya kimwili dhidi ya asili ya dhambi iliyo ndani yetu, ikitusukuma kukubali mvuto wa majaribu. Pambano hilo halikomi baada ya kuwa Mkristo.
   

3.

Je, ushindi unawezekana, na kutoka wapi? I Wakorintho 15:57





Kumbuka: Bwana asifiwe! Ingawa majaribu yanaweza kuwaka, ushindi unaweza kupatikana—kupitia Kristo! Jitahidi kudumu kumtazama Yeye.
   

4.

Ipi hatua gani ya kwanza ya kuchukua tunapojikwaa na kushindwa majaribu fulani?

Mithali 28:13




I Yohana 1:9




Kumbuka: Mara nyingi sana mwitikio wetu wa asili ni kukataa, kutoa udhuru, kuhalalisha, au kupunguza unyeti wa tabia yetu. Lakini uhuru huja tu kwa kuukabili vilivyo ukweli unaotuhusu sisi wenyewe. Kama ambavyo Yesu aliwahi kusema, “Mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru." (Yohana 8:32)
   

5.

Paulo alifafanuaje toba ya kweli? II Wakorintho 7:10-11






Kumbuka: Toba ni zaidi ya kukiri dhambi tu; ni huzuni ya kina kwa ajili ya dhambi, na nia thabiti ya kuiacha. Toba ya namna hii inatoka kwa Mungu pekee—kwa hivyo ukijikuta unapambana na dhambi fulani unayoipenda, omba karama ya toba ya kweli.
   

6.

Mungu anaitikiaje maungamo na toba ya kweli? Zaburi 103:10-14







Kumbuka: Mungu yuko tayari kabisa kusamehe—na kututendea kana kwamba hatujawahi kufanya dhambi. Swali gumu zaidi, mara nyingi, ni iwapo tuko tayari kujisamehe sisi wenyewe na kuikubali zawadi ya bure ya Mungu ili tuanze upya.
   

7.

Je, tunapaswa kuomba nini tena baada ya kujikwaa katika dhambi?

Zaburi 51:10



Ezekieli 36:27



II Wakorintho 5:17



Kumbuka: Neno la Mungu limejaa ahadi za pekee ajabu kwa ajili ya ushindi dhidi ya dhambi. Shikilia aya hizi na kuzidai kwa ajili yako!
   

8.

Kwa mujibu wa Petro, ahadi za Neno la Mungu zinaweza kufanya nini? II Petro 1:4. Angalia pia Zaburi 119:11




Kumbuka: Ahadi za Maandiko ni kiini cha kuepuka majaribu! Zinapohifadhiwa moyoni, na kuchanganywa na imani—nguvu ya dhambi inavunjwa.
   

9.

Je, unadhani Mungu yuko radhi kukusamehe mara ngapi? Mathayo 18:21-22




Kumbuka: Ingawa Mungu ni mtakatifu na anatarajia utii, Yeye pia ni mvumilivu na anaikumbuka silika yetu, kwamba sisi ni mavumbi. Hata kama umejikwaa tena na tena—weka tumaini lako kwa Mungu. Mtafute kwa moyo wako wote, na ushindi utakuja. Yeremia 29:12-13.
   

10.

Je, hatimaye Mungu atakuwezesha kufanya nini? Yuda 1:24






Rafiki, hivi kuna dhambi fulani maishani mwako inayosababisha hatia? kuchanganyikiwa? mfadhaiko? Usikate tamaa! Ushindi unawezekana kupitia Kristo, na kwa wakati timilifu wa Mungu na kwa njia Yake ya upole, atakufunulia kile unachohitaji kujua ili ushinde. Kwa sasa, kuwa mwaminifu, ungama dhambi yako kwa Mungu, na utubu. Kisha shikilia Neno la Mungu—ahadi Yake ya kusamehe na ahadi Yake ya kutakasa. Hizi mbili ni muhimu sana ikiwa unataka kuokoka! Je, uko tayari kusonga mbele kwa ujasiri usiopungua katika vita vyako binafsi dhidi ya majaribu?



Ndiyo              Hapana

Kukabili Jaribu

Survival Kit > Juma 3 > Mapendekezo Kutendea Kazi

Je, uko tayari kupata dondoo zaidi za kuikariri Biblia? Juma hili tutaangalia kanuni zingine mbili muhimu: jinsi ya kuhamisha aya fulani kutoka kwenye hifadhi zako za kumbukumbu za muda mfupi hadi kwenye kumbukumbu zako za kudumu, na kisha jinsi ya kukumbuka marejeleo—mahali ambapo aya hiyo inapatikana. Fuata mapendekezo haya kwa uangalifu, nayo yataleta mabadiliko makubwa katika kukariri kwako.

Dondoo #5. Jikite Kuhifadhi.


Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno Yangu; shika amri Zangu ukaishi. Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; wala usiyakatae maneno ya kinywa Changu. Mithali 4:4-5

Mungu anatutaka siyo tu kulikariri Neno Lake, lakini “kulichimbia” akilini mwetu. Anataka tulihifadhi, tulidumishe, tulishikilie sana, na kutolisahau kamwe. Tunapaswa “kuzingatia kwa dhati” aya zetu, “tusije tukaziacha zitoweke” (Waebrania 2:1). Hata hivyo, kwa nini uwekeze muda wa kukariri aya fulani ambayo utakuja kuisahau siku moja au mbili baadaye? Siri, bila shaka, ni mfumo madhubuti wa kuduria rudia. Hiki hapa tunachoshauri:

Mara baada ya kukariri aya fulani, iwekee tarehe, na kuichanganya pamoja na aya zingine zilizokaririwa hivi karibuni katika moja ya mifuko ya ndani ya kifurushi chako cha aya. (Mfuko mwingine ni wa kadi tupu). Rudia kundi hili la aya kila siku—hususan muda wako wa kujifunza asubuhi. Usikose hata siku moja! Angalia upande wa kadi wenye marejeleo pekee, nukuu aya hiyo, kisha geuza kadi ili kuangalia usahihi wako. Baada ya majuma kadhaa aya hiy itakuwa rahisi kunukuu—lakini usiishie hapo! Itachukua muda wa miezi miwili kamili ili kuifanya aya husika idumu kabisa kwenye ubongo wako.

Mara tu tarehe inapoonesha kwamba aya imekuwa katika marudio yako kila siku kwa miezi miwili, ihamishie kwenye faili la marudio ya kudumu unayoihifadhi nyumbani. Fanyia kazi aya hizi angalau mara moja kwa juma, mwanzoni. Baadaye, unapokuwa umekusanya aya mia kadhaa, unaweza kuamua kuhamisha aya zako zinazojulikana vizuri kwenda sehemu ya kurudia ya kila mwezi. Endelea kufanya hivi daima, na kila aya itakuwa madhubuti, kwenye ncha ya ulimi wako. Na kama aya fulani ikisahaulika kidogo, ipatie uangalifu zaidi: iingize kwenye marudio yako ya kila siku au juma kwa muda. Punde itachipuka uhai—safi kama zamani!


Ili kukusaidia katika kukariri, FAST ina nyenzo madhubuti ya kurudia ambayo hurahisisha mchakato mzima wa rudia. Tunaipendekeza sana. Kwa maelezo zaidi, iangalie katika WWW.FAST.ST/ENGINE.

Hebu fikiria: ukikariri aya mbili kwa juma, na kutumia mfumo fanisi wa rudia, utakuwa na aya zaidi ya mia moja katika muda usiozidi mwaka mmoja. Katika miaka kumi utakuwa na zaidi ya elfu! Hebu fikiria—aya elfu moja zote zikiwa zimehifadhiwa kikamilifu akilini mwako, na kwenye ncha ya ulimi wako! Inaweza kutokea.

Dondoo #6. Jua Marejeleo Yako.


Jitahidi kujionesha kwamba umekubaliwa na Mungu, mtendakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kihalali neno la kweli. II Timotheo 2:15   

Hupaswi kujua tu kile ambacho aya fulani inasema—lakini pia mahali inapopatikana. Haitoshi kuweza kuinukuu, lazima uweze kuifungua katika Biblia yako na kumwonesha rafiki. Watu wengi wanahangaika kukumbuka marejeleo, lakini siyo ngumu sana, kama utafuata tu mapendekezo haya rahisi:

Kwanza, hakikisha umejifunza marejeleo ya aya husika. Njia moja ya kufanya hivyo ni kile ninachokiita “gundi ya marejeleo.” Kimsingi, jaribu kusema rejeleo, na sehemu ya kwanza tu ya aya hiyo haraka, mara kumi au zaidi—hadi inaponata akilini. Kisha rudia mara nyingi kadiri inavyohitajika. Kimsingi, inasikika hivi:

     I Yohana 1:9, Tukiziungama dhambi zetu...
     I Yohana 1:9, Tukiziungama dhambi zetu...
     I Yohana 1:9, Tukiziungama dhambi zetu...

Pili, unapofanya marudio yako ya kila siku, kila mara nukuu rejeleo kabla na baada ya aya husika—kila wakati. Ifikirie kama sandwichi: rejeleo, aya, rejeleo. Hii inaishikamanisha aya kwenye rejeleo na kinyume chake. Kwa hiyo unaposikia rejeleo, unaifikiria aya hiyo. Na unapoisikia aya, unafikiria rejeleo. Inafanya kazi!

Na tatu, hata jambo la kufurahisha zaidi, nyenzo yetu ya kurudia ina mazoezi maalum ya marejeleo unayoweza kufanya ili kuyakumbuka vizuri maeneo hayo yote ya aya. Jaribu!

Kujua marejeleo ya aya zako ni sehemu muhimu ya kukariri kwako. Fuata vidokezo hivi na utakuwa na hakika ya kufanikiwa.