![]() |
Dokezo:Habari! Karibu tena kwenye Nyenzo za Usalama za FAST. Tunaomba kwamba programu hii ikupe maarifa muhimu kuhusu maisha ya Kikristo yenye furaha. Maarifa yanayoleta mabadiliko halisi. Maarifa yenye ufanisi. Juma hili utajifunza siri ya nguvu katika maisha ya Kikristo. Mtume Paulo aliwahi kusema “ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku” (2 Wakorintho 4:16). Ilikuwepo nguvu ya ndani iliyomwezesha Paulo kuvumilia hali ngumu zaidi kwa ushindi. Na nguvu hiyo inapatikana kwetu! Inakuja kupitia ushirika pamoja na Kristo. Pia utajifunza baadhi ya kanuni za ziada za kutunza kumbukumbu ya Maandiko. Petro anasema Neno la Mungu ni mbegu isiyoharibika, na kwamba linaishi na kudumu milele. (1 Petro 1:23). Siyo kitabu chako cha kawaida! Lakini kama mbegu zote, lazima ipandwe. Lazima izame ndani kabisa moyoni mwetu, ikiwa inapaswa kuota. Fikiria hilo. Kumbukumbu ya Maandiko ni kupanda mbegu hai, isiyoharibika. Mhariri, Amefichwa katika Kristo |
| Jina: | Saini: | ||
| Tarehe: |
![]() |
Ulifanyaje katika Uchunguzi wako wa kwanza wa Biblia? Juma hili Uchunguzi wetu wa Biblia unaitwa Kumtazama Yesu. Unatafiti maana hasa ya kumfuata Kristo. Kabla hujaanza, hakikisha unamwomba Mungu akuoneshe mambo makuu katika Neno. Dai ahadi ya Yeremia 33:3. Inapendeza ilioje kwamba Mwasisi halisi wa kitabu hicho anapatikana ili kukielezea! |
![]() |
Aya yako ya kukariri juma hili ni Yohana 15:5. Iandike kwenye kadi, iweke kwenye mfuko wa nje wa kifurushi chako cha aya, na kuweka aya ya juma lililopita kwenye mfuko wa ndani. Unapofanyia kazi aya yako mpya, hakikisha hausahau ile ya zamani. Zipitie upya zote mbili angalau mara moja kila siku—hadi uweze kuzinukuu zote kwa usahihi. |
![]() |
Mapendekezo Yako Kutendea Kazi juma hili hukupa vidokezo viwili miongoni mwa dondoo mbili za kumbukumbu zinazosisimua zaidi. Yanazungumzia jinsi ya kupata maana kutoka kwenye aya na kisha kuiunganisha na maisha ya kila siku ya mtu husika. Mtu anapojifunza kutafakari Maandiko na kuyatumia kivitendo, Biblia inakuwa kitabu kipya kabisa! Durusu dondoo hizi kila siku, pamoja na zile mbili za kwanza—hadi uweze kukariri zote nne kwa mpangilio. |
1. |
Yesu alisema nini kinapaswa kumtokea kila mtu? Yohana 3:3 Kumbuka: Dhahamu (uzoefu) ya kuzaliwa upya hauepukiki kabisa kwa maisha ya Kikristo. Kama ambavyo Yesu aliendelea kueleza: “kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho!" |
2. |
Alipoulizwa, “Mambo haya yanawezekanaje?” Yesu alitumia kisa kutoka Agano la Kale ili kuelezea kuzaliwa upya. Kisa hicho kilikuwa kipi? Yohana 3:14-15 Kumbuka: Yesu alitumia kisa cha kale katika siku za Musa ili kuonesha ukweli wa kina wa kiroho jinsi mwanadamu anavyozaliwa mara ya pili! |
3. |
Je, ni dondoo gani ya “usalama” katika kisa alichorejelea Yesu? Hesabu 21:8-9 Kumbuka: Ingawa “imani” na “kusadiki” wakati mwingine ni dhana zisizo wazi, neno “angalia” ni rahisi kueleweka. Kwa asili tunatambua maana ya kugeuza macho na kutazama. |
4. |
Jinsi gani kila moja ya aya zifuatazo huielezea kanuni hiihii? Isaya 45:22 Waebrania 12:1-2 II Wakorintho 3:18 Kumbuka: Tena na tena tunaagizwa kutazama tu. Njoo uone! |
5. |
Ni njia gani moja ambayo kwayo tunaweza kudumisha fikra zetu za kiroho kwa Yesu? Yohan 5:39 Kumbuka: Ingawa hatuwezi kumwona Yesu kiumbile, tunaweza kuichunguza Biblia na kudumisha mtazamo wetu katika maisha Yake kupitia Neno. Maandiko ni kama kioo kinachomwakisi Kristo kwa wote wanaotazama. Angalia II Wakorintho 3:18. |
6. |
Nini matokeo ya kukutana na Kristo kupitia Maandiko? Luka 24:32 Kumbuka: Ingawa kuna sababu nyingi za kujifunza—ile iliyo muhimu zaidi ni uzoefu wa ushirika pamoja na Kristo, kuimarisha na kuchangamsha moyo. |
7. |
Ni mara ngapi tunapaswa kuwa na aina hii ya kukutana? II Wakorintho 4:16 Kumbuka: Usalama wetu kiroho unategemea juhudi zetu kila siku kuutafuta ushirika pamoja na Kristo kupitia maombi na kujifunza Neno Lake! |
8. |
Kwa mujibu wa aya zifuatazo, kwa nini kufanywa upya nia kila siku ni muhimu sana? Warumi 12:2 II Wakorintho 4:16-18 Waefeso 4:23-24 Kumbuka: Uaminifu wetu katika kumtazama Kristo na uzoefu kila siku kufanywa upya nia yetu ni dondoo ya mabadiliko ya maisha yetu. Hatupaswi kamwe kupoteza mtazamo wa ukweli huu muhimu! |
9. |
Je, tunapaswa kuweka kipaumbele gani katika kumtazama Kristo? Zaburi 27:4 Wafilipi 3:8 Kumbuka: Kama ambavyo Paulo aliwahi kuandika, “kwangu mimi kuishi ni Kristo” (Wafilipi 1:21). Sote tunapaswa kujitahidi kuifikia hatua hii. |
10. |
Tutajifunza somo gani kwa kumweka Kristo awe wa kwanza? Wafilipi 4:13 |
![]() |
Ndiyo | ![]() |
Hapana |
Yatafakari mambo haya; jikabidhi kabisa kwayo; ili maendeleo yako yawe dhahiri kwa wote. I Timotheo 4:15
Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Yakobo 1:22