Kumtazama Yesu

Survival Kit > Juma 2 > Dokezo

     

Dokezo:


Habari! Karibu tena kwenye Nyenzo za Usalama za FAST. Tunaomba kwamba programu hii ikupe maarifa muhimu kuhusu maisha ya Kikristo yenye furaha. Maarifa yanayoleta mabadiliko halisi. Maarifa yenye ufanisi.

Juma hili utajifunza siri ya nguvu katika maisha ya Kikristo. Mtume Paulo aliwahi kusema “ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku” (2 Wakorintho 4:16). Ilikuwepo nguvu ya ndani iliyomwezesha Paulo kuvumilia hali ngumu zaidi kwa ushindi. Na nguvu hiyo inapatikana kwetu! Inakuja kupitia ushirika pamoja na Kristo.

Pia utajifunza baadhi ya kanuni za ziada za kutunza kumbukumbu ya Maandiko. Petro anasema Neno la Mungu ni mbegu isiyoharibika, na kwamba linaishi na kudumu milele. (1 Petro 1:23). Siyo kitabu chako cha kawaida!

Lakini kama mbegu zote, lazima ipandwe. Lazima izame ndani kabisa moyoni mwetu, ikiwa inapaswa kuota. Fikiria hilo. Kumbukumbu ya Maandiko ni kupanda mbegu hai, isiyoharibika.

Mhariri,
Amefichwa katika Kristo

These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST

Kumtazama Yesu

Survival Kit > Juma 2 > Malengo


Jina:                                                     Saini:                                         
Tarehe:                                         


Ulifanyaje katika Uchunguzi wako wa kwanza wa Biblia? Juma hili Uchunguzi wetu wa Biblia unaitwa Kumtazama Yesu. Unatafiti maana hasa ya kumfuata Kristo. Kabla hujaanza, hakikisha unamwomba Mungu akuoneshe mambo makuu katika Neno. Dai ahadi ya Yeremia 33:3. Inapendeza ilioje kwamba Mwasisi halisi wa kitabu hicho anapatikana ili kukielezea!

Aya yako ya kukariri juma hili ni Yohana 15:5. Iandike kwenye kadi, iweke kwenye mfuko wa nje wa kifurushi chako cha aya, na kuweka aya ya juma lililopita kwenye mfuko wa ndani. Unapofanyia kazi aya yako mpya, hakikisha hausahau ile ya zamani. Zipitie upya zote mbili angalau mara moja kila siku—hadi uweze kuzinukuu zote kwa usahihi.

Mapendekezo Yako Kutendea Kazi juma hili hukupa vidokezo viwili miongoni mwa dondoo mbili za kumbukumbu zinazosisimua zaidi. Yanazungumzia jinsi ya kupata maana kutoka kwenye aya na kisha kuiunganisha na maisha ya kila siku ya mtu husika. Mtu anapojifunza kutafakari Maandiko na kuyatumia kivitendo, Biblia inakuwa kitabu kipya kabisa! Durusu dondoo hizi kila siku, pamoja na zile mbili za kwanza—hadi uweze kukariri zote nne kwa mpangilio.


Kuingia kwa maneno Yako nafsini kwatia nuru;
Humpatia ufahamu mjinga.
Zaburi 119:130


Kumtazama Yesu

Survival Kit > Juma 2 > Uchunguzi wa Biblia

Ulifanyaje kwenye Uchunguzi wako wa kwanza wa Biblia? Ni muhimu kwa maisha yetu ya Kikristo kwamba tuwe na imani ya kweli katika hamu ya Mungu ya kufanya mambo makuu kwa ajili yetu katika maisha yetu! Somo hili linaangazia ufunguo muhimu vilevile linalohusu usalama wa Mkristo—nguvu kufanywa upya ya nia iliyojikita kwa Kristo. Anza somo kwa maombi, na ufurahie somo lako.

Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani Yangu Nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo Mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote. Yohana 15:5


1.

Yesu alisema nini kinapaswa kumtokea kila mtu? Yohana 3:3






Kumbuka: Dhahamu (uzoefu) ya kuzaliwa upya hauepukiki kabisa kwa maisha ya Kikristo. Kama ambavyo Yesu aliendelea kueleza: “kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho!"
   

2.

Alipoulizwa, “Mambo haya yanawezekanaje?” Yesu alitumia kisa kutoka Agano la Kale ili kuelezea kuzaliwa upya. Kisa hicho kilikuwa kipi? Yohana 3:14-15







Kumbuka: Yesu alitumia kisa cha kale katika siku za Musa ili kuonesha ukweli wa kina wa kiroho jinsi mwanadamu anavyozaliwa mara ya pili!
   

3.

Je, ni dondoo gani ya “usalama” katika kisa alichorejelea Yesu? Hesabu 21:8-9






Kumbuka: Ingawa “imani” na “kusadiki” wakati mwingine ni dhana zisizo wazi, neno “angalia” ni rahisi kueleweka. Kwa asili tunatambua maana ya kugeuza macho na kutazama.
   

4.

Jinsi gani kila moja ya aya zifuatazo huielezea kanuni hiihii?

Isaya 45:22



Waebrania 12:1-2



II Wakorintho 3:18



Kumbuka: Tena na tena tunaagizwa kutazama tu. Njoo uone!
    

5.

Ni njia gani moja ambayo kwayo tunaweza kudumisha fikra zetu za kiroho kwa Yesu? Yohan 5:39






Kumbuka: Ingawa hatuwezi kumwona Yesu kiumbile, tunaweza kuichunguza Biblia na kudumisha mtazamo wetu katika maisha Yake kupitia Neno. Maandiko ni kama kioo kinachomwakisi Kristo kwa wote wanaotazama. Angalia II Wakorintho 3:18.
   

6.

Nini matokeo ya kukutana na Kristo kupitia Maandiko? Luka 24:32





Kumbuka: Ingawa kuna sababu nyingi za kujifunza—ile iliyo muhimu zaidi ni uzoefu wa ushirika pamoja na Kristo, kuimarisha na kuchangamsha moyo.
   

7.

Ni mara ngapi tunapaswa kuwa na aina hii ya kukutana? II Wakorintho 4:16





Kumbuka: Usalama wetu kiroho unategemea juhudi zetu kila siku kuutafuta ushirika pamoja na Kristo kupitia maombi na kujifunza Neno Lake!
   

8.

Kwa mujibu wa aya zifuatazo, kwa nini kufanywa upya nia kila siku ni muhimu sana?


Warumi 12:2



II Wakorintho 4:16-18



Waefeso 4:23-24



Kumbuka: Uaminifu wetu katika kumtazama Kristo na uzoefu kila siku kufanywa upya nia yetu ni dondoo ya mabadiliko ya maisha yetu. Hatupaswi kamwe kupoteza mtazamo wa ukweli huu muhimu!
   

9.

Je, tunapaswa kuweka kipaumbele gani katika kumtazama Kristo?

Zaburi 27:4



Wafilipi 3:8



Kumbuka: Kama ambavyo Paulo aliwahi kuandika, “kwangu mimi kuishi ni Kristo” (Wafilipi 1:21). Sote tunapaswa kujitahidi kuifikia hatua hii.
   

10.

Tutajifunza somo gani kwa kumweka Kristo awe wa kwanza? Wafilipi 4:13






Imesemwa kwamba neno “Mkristo” kimsingi humaanisha mtu aliye na "Kristo ndani" yake, na ni kweli. Lakini kwa wengi, kuna nguvu halisi kidogo. Siri ya kufurahia maisha halisi ya Kikristo ni kujifunza kudumisha macho yetu yamwelekee Yesu. Siku baada ya siku, lichunguze Neno, kutana na Kristo, na ruhusu moyo wako upate joto. Ukifanya hivyo, punde utajigundua unakua zaidi na zaidi ili kufanana na Mwokozi. Utafahamu kwa uwazi zaidi, utegemezi wako mkuu Kwake na uwezo wako mkuu ndani Yake. Kristo atakuwa kiini cha maisha yako—na itakuwa dhahiri kwa kila mmoja anayekuzunguka. Hivi hiyo ni shauku ya moyo wako?



Ndiyo              Hapana

Kumtazama Yesu

Survival Kit > Juma 2 > Mapendekezo Kutendea Kazi

Juma hili tutakuwa tukiangalia dondoo mbili muhimu zaidi katika kukariri Maandiko kwa ufanisi. Unaona, haitoshi tu kujua jinsi ya kukariri aya fulani—lazima pia ujifunze jinsi ya kutambua maana ya aya hiyo, na kisha uingize aya hiyo maishani mwako. Stadi hizi zinaitwa tafakari na matumizi. Tunaomba kwamba upate manufaa ya mapendekezo hapa chini.

Dondoo #3. Jifunze Kutafakari.


Yatafakari mambo haya; jikabidhi kabisa kwayo; ili maendeleo yako yawe dhahiri kwa wote. I Timotheo 4:15

Baadhi ya baraka kuu zaidi katika Biblia zimeahidiwa kwa wale wanaojifunza kutafakari Maandiko mchana na usiku. Wale wanaofikiria daima kile ambacho aya fulani inasema. Ili kufanya hivi hakika huhitaji kukariri—si mara zote Biblia yako imefunguliwa mbele yako—lakini unahitaji mengi zaidi. Lazima ujifunze jinsi ya kutafuna aya, kwa maombi, na kubaini kanuni zilizomo ndani yake. Haya hapa baadhi ya mapendekezo:





Dondoo #4. Tumia Neno.


Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Yakobo 1:22

Kutafakari kunapaswa daima kuunganishwa na matumizi binafsi. Matumizi kimsingi ni kuchukua kanuni unazoziona katika aya, na kisha kutafuta njia za kuzitekeleza. Hutafuta kujumuisha aya fulani katika maisha ya mtu ya kila siku. Hutafuta hatua halisi za kuiweka aya katika vitendo. Lengo lake ni uzoefu wa aya husika. Hivi hapa vidokezo kadhaa vya kukufanya uanze:





Mwombe Mungu akufahamishe angalau mradi mmoja kwa kila aya unayokariri—kitu fulani kidogo unachoweza kufanya ili kusaidia kuifanyia kazi aya hiyo maishani mwako. Jaribu kuhakikisha kwamba miradi hii imeunganika dhahiri na aya unayokariri, kwamba ni mahususi, na kwamba ni midogo kiasi cha kutosha kutekelezwa siku hiyo au punde baadaye.