Ufuatiliaji Madhubuti
Revival Keys > Juma la 9 > Dokezo
 |
|
Dokezo:
Hili hapa, somo letu la mwisho. Na labda lenye changamoto zaidi! Ndani yake, tunajikita katika uamsho wa mwisho duniani. Kile ambacho wakati mwingine tunaita mvua ya masika. Kile ambacho kitawawezesha watu wa Mungu waimalize kazi. Kutangaza kilio kikuu mwishowe. Je, huitamani na kuitazamia siku hiyo?
Kwa kweli, ndiyo kile ambacho tumekuwa tukizungumzia wakati wote. Siyo matukio yale ya “kawaida” ya uamsho ambao kanisa umefurahia kwa karne nyingi, ndiyo tuyatakayo, bali aina tofauti ya uamsho. Ile iliyojengwa juu ya kanuni thabiti za kibiblia. Ile ambayo hustahimili na kuimarika zaidi kuliko ile inayofifia na kutoweka. Ile ambayo ina uwezo wa kuenea kila mahali. Hadi mwishowe dunia yote inapokuwa imegubikwa utukufu wake.
Uamsho huo unakuja. Na ni hivi karibuni. Hebu tukusudie kufanya kazi ya kuutafuta kwa akili—na tuwe tayari kwa tukio hilo, linapokuja...
Mhariri,
Amefichwa katika Kristo |
These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST
Ufuatiliaji Madhubuti
Revival Keys > Juma la 9 > Malengo
| Jina: |
|
|
Imesainiwa na: |
| Tarehe: |
|
 |
Uchunguzi wako wa mwisho wa Biblia ni wa kina. Mathayo 25:1-13. Ni mfano unaofahamika vyema, lakini unastahili kuzingatiwa kwa uangalifu zaidi. Alama zote zinawakilisha nini? Ni onyo gani ambalo Yesu alikuwa akijaribu kutoa? Linakuambia nini kuhusu uamsho wa mwisho duniani? |
 |
Utavutiwa sana na mada yetu ya mwisho kuhusu mapendekezo ya kivitendo: Mvua ya Masika. Ndani yake utapata dondoo kadhaa makini zinazogusia uamsho ambao hakika utaufurahisha moyo wako... |
 |
Kuhusu aya yako ya mwisho ya kukariri juma hili, jifunze Ufunuo 18:1. Ni unabii wenye nguvu, na utimizo wake uko mbeleni tu kwa watu wa Mungu. Njoo kwenye mkutano unaofuata wa timu ukiwa umejiandaa kuinukuu pamoja na aya zote ambazo umepangiwa hadi sasa. Dhamiria kukamilisha kozi hii ukijua kila aya kwa usahihi! |
 |
Na kwa mara ya mwisho, tunataka kukuhimiza uombee uamsho: kwa ajili yako, kwa ajili ya timu yako, na kwa ajili ya kanisa lako. Na hasa uombee uamsho wa mwisho. Unganisha maombi yako na maelfu ya wengine kote ulimwenguni wanaomba kila siku ili mvua ya masika ije! |
FAST
Kukamilisha Jukumu Takatifu
Ufuatiliaji Madhubuti
Revival Keys > Juma la 9 > Kuchunguza Maandiko
Mada: Mathayo 25:1-13
Muhtasari:
Maoni/Dondoo:
Kanuni & Matumizi:
Wazo Kuu:
Ufuatiliaji Madhubuti
Revival Keys > Juma la 9 > Mapendekezo ya Kivitendo
Mvua ya Masika
Tumejifunza mengi kadiri tuliposhughulikia masomo mbalimbali katika kozi hii ya Funguo za Uamsho. Tumeangalia hitaji letu la haraka la uamsho, masharti muhimu ya uamsho, jinsi ya kuamsha uamsho, kuulinda, na kuhakikisha unaenea. Na tumekuhimiza uone uwezo wako kama wakala wa uamsho. Lakini kozi hii inakaribia mwisho, na tunataka kukuachia mawazo machache ya uamsho tunapoagana. Na kwa namna mahususi, uamsho wa mwisho duniani. Mvua ya masika.
Unaona, historia ya kanisa la Kikristo imejaa matukio halisi ya uamsho nyakati zote katika miaka 2000 iliyopita. Matukio makuu ya uamsho wa kiroho, harakati, kumiminiwa kwa Roho. Lakini zote zina jambo moja linalofanana: matukio yote yamekuja na kuondoka. Huwaka sana mahali fulani kwa muda, kisha hufifia. Huenda yakaenea kidogo, au kudumu kitambo kidogo—lakini bila shaka hudorora na kutoweka. Hizi zote zimekuwa mvua za vuli.
Uamsho wa mwisho utakuwa tofauti. Huanzia mahali fulani, labda maeneo kadhaa wakati mmoja—lakini kisha huendelea kuwaka mno. Badala ya kutoweka, kwa kweli huimarika. Na huanza kuenea. Hapa na pale, kidogo kidogo, kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kama moto mkali, huruka kila mpaka, kila ukingo, kila kizuizi. Huthibitika kwamba haiwezekani kuuzuia, na ulimwengu wote unagubikwa mwishowe. Hadi kila sehemu ya dunia hii imewaka moto. Wengi wataikataa baraka hii, lakini hakuna yeyote atakayeepuka matokeo yake.
Na hata wakati huo, rehema inapoanza kufungwa, na watu wa Mungu wakiingia katika matukio ya mwisho ya kujaribiwa yanayobainishwa katika Ufunuo, uamsho huu hukataa kufifia hata kidogo, bali badala yake, huzidi kuangaza sana. Kwa kweli, ni tukio hili la mwisho la kumwagwa Roho ndilo huwatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya zahama inayokaribia.
Mvua ya masika itakuwa harakati ya kilimwengu ya nguvu isiyoweza kufikirika. Uamsho wa mwisho duniani hautafanana na chochote ambacho tumeona hadi sasa...
Mantiki Husika
Haya yote hupendekeza kwamba tutahitaji kuuelewa uamsho kikamilifu zaidi. Ili kushiriki katika mvua ya masika, tutalazimika kujifunza jinsi ya kushirikiana na Mungu kikamilifu zaidi. Ili kutambua michakato ya kujazwa Roho, kuongozwa na Roho, kuwezeshwa na Roho. Tutalazimika kuwa na akili zaidi kuhusu nini maana ya uamsho na jinsi unavyofanya kazi.
Kwa upande mmoja lazima tujue jinsi ya kufunga na kuukaza mlango dhidi ya kila aina ya ushupavu. Lakini kwa upande mwingine, lazima tujifunze jinsi ya kumpa Roho Mtakatifu fursa kamili, isiyo na vikwazo ili aingie mioyoni mwetu. Tutahitaji kuelewa jinsi ya kutambua uzoefu halisi, kuutunza, kuukuza, kuuimarisha, na hatimaye, kuwashirikisha wengine.
Baadhi ya mada hizi tumezigusia katika kozi hii ya Funguo za Uamsho, lakini tumetumbukiza tu vidole vyetu kwenye bahari ya uzoefu wa kina zaidi. Kabla Mungu hajatukasimisha onesho kamili la mwisho la nguvu ambayo ameahidi, tutalazimika kujifunza mengi zaidi...
Uamsho wa Mwisho
FAST imekuwa huduma iliyojengwa katika uamsho tangu ilipoanzishwa. Na tumewasaidia maelfu ya watu kupata uamsho kupitia nyenzo zetu mbalimbali za mafunzo. Siyo kwa sababu kuna lolote maalum kuhusu huduma yetu, bali kwa sababu kuna nguvu katika Neno la Mungu. Na tumedumu kwenye lengo la kuwapa watu nyenzo za kuyafahamu Maandiko.
Lakini kwa miaka mingi tumetafakari pia juu ya uamsho huu wa mwisho unaokuja. Kuhusu Mvua ya Masika itakuwaje. Na tumekusanya dondoo chache njiani. Kanuni ambazo wewe pia unaweza kugundua kwamba zina msaada. Hizi hapa chache za haraka:
Haitatokea kwa Nasibu
RaBadala ya kutokea yenyewe, mvua ya masika itaingiwa kwa makusudi, kwa kudhamiria. Mungu atakuwa na watu wanaoelewa masharti ya uamsho, na kuiandaa njia kwa makini.
Haitakuwa ya Kimhemko Tu
Matukio mengi ya uamsho zamani yamekuwa yakisheheni mihemko. Mvua ya masika itakuwa yenye kanuni, iliyojikita hasa katika Maandiko. Itatafutwa kwa utulivu, na kwa busara.
Haitakuwa ya Msisimko
Uamsho wa aina hii hauhusu maonesho ya nje au udhihirisho wa nje. Badala yake, mvua ya masika huongoza kwenye toba tulivu, na kujisalimisha kwa Mungu. Hujenga badiliko la kina la ndani.
Haitasababisha Ushupavu wa Kidini
Ingawa daima watakuwepo watu wanaoenenda kimheuko, mvua ya masika huwaleta watu katika utaratibu, umoja, upatanifu. Huwavuta watu kwenye maisha ya uwiano halisi wa kibiblia.
Haitafukuzia Nuru Mpya
Ingawa maarifa na uvumbuzi mkuu mara nyingi hufanywa wakati wa uamsho, hizi kamwe hazipingani au hazitupeleki mbali na ukweli uliothibitika. Badala yake, mvua ya masika itatufanya tujikite zaidi kutekeleza Maandiko maishani mwetu.
Haitashambulia Kanisa la Mungu
Kanisa ndicho chombo ambacho Mungu hukipatia heshima ya juu. Mitazamo mibaya hutokana na ukosefu wa imani katika uwezo wa Mungu wa kuhuisha na kurejesha. Mvua ya masika hutujaza tumaini, kwa kutarajia uamsho mkuu.
Haitatufanya Tuwe Jeuri
Badala ya kutufanya tuwe wakali au wakatili dhidi ya wengine, mvua ya masika itatujaza upendo kwa waumini wenzetu, na kutufanya tuwe watumishi wanyenyekevu na waelekevu.
Haitapuuza Uinjilisti
Badala ya kuelekeza nguvu zetu kwa waumini wengine, mvua ya masika itatushurutisha kuifikia jamii yetu, kuzifikia roho zilizopotea ili zimrudie Kristo. Hutupatia uwezo wa kuimaliza kazi. Na mwisho...
Haitakuwa na Mawazo Duni
Ingawa hatutapuuza uamsho binafsi au mahalia, mvua ya masika ni harakati ya kilimwengu iliyokusudiwa kuleta mabadiliko ulimwenguni. Tutahisi kushurutishwa kuwezesha, kuratibu, na kuunga mkono harakati za uamsho kote ulimwenguni.
Bila shaka kuna masomo mengine mengi zaidi ya kujifunza kuhusu uamsho. Kadiri tunavyokaribia ule mwisho, ndivyo tutakavyoelewa zaidi jinsi Roho Mtakatifu anavyofanya kazi. Na kadiri tunavyokuwa na akili zaidi, ndivyo Mungu anavyoweza kumimina nguvu Zake.
Wazo Moja la Mwisho
Hili hapa wazo moja la mwisho. Hatuwezi kuendelea kusukumia mbali mvua ya masika hadi wakati fulani katika siku zijazo. Biblia inaweka wazi, kwamba tunapofikia wakati katika historia ya dunia ambapo tunahitaji mvua ya masika, tunapaswa kuiomba (Zekaria 10:1). Na kwamba tukiiomba, Mungu atatupatia. Siyo wakati fulani katika siku zijazo, siyo kesho, bali leo.
Naamini wakati huo umewadia. Iwapo unaamini pia, hivi hutaazimu kuomba kwa ajili ya tukio hili la mwisho la kumwagwa Roho wa Mungu? Na kuyaishi maisha YAKO kama wakala wa uamsho?
Ufuatiliaji Madhubuti
Revival Keys > Juma la 9 > Uhakiki wa Mwisho
Ili kukamilisha programu hii, tafadhali thibitisha kukamilisha malengo yafuatayo:
Aya za Kukariri
Waefeso 5:14
Zaburi 119:18
Mithali 20:27
Waebrania 3:13-14
Yohana 4:35
Luka 11:13
Waebrania 6:11-12
Isaya 49:6
Ufunuo 18:1
Kuchunguza Biblia
Weka tiki hapa ikiwa umekamilisha mazoezi yote tisa ya Uchunguzi wa Biblia
Mapendekezo ya Kivitendo
Masharti ya Uamsho
Kulichunguza Neno
Katika Kujibu Maombi
Mausia Yenye Faraja
Moyo wa Huduma
Mkakati wa Uamsho
Nguvu ya Timu
Mawakala wa Uamsho
Mvua ya Masika
Nyenzo za Ziada
Weka tiki hapa ikiwa umesoma Nyenzo za Ziada nane zote
Hongera! Sasa umekamilisha Funguo za Uamsho za FAST! Tunatumai Mungu amebariki sana juhudi zako za kuelewa jinsi ambavyo Roho wa Mungu anafanya kazi kikamilifu zaidi. Na tunakuhimiza ukabidhi maisha yako kuwa wakala wa uamsho!
Je, programu hii imekuwa baraka kwako? Kwa nini usitutumie dokezo fulani, na utueleze jinsi ambavyo imebadilisha maisha yako? Asante!