Mabomu Yatembeayo
Revival Keys > Juma la 8 > Dokezo
 |
|
Dokezo:
Ni ngumu kuamini, lakini tunakaribia mwisho wa kozi hii. Somo moja baada ya hili, nawe utakuwa mhitimu mwingine wa Funguo za Uamsho! Lakini usifikiri kwamba mambo yanaisha. Tumehifadhi masomo yetu mawili bora kabisa yawe mwishoni!
Juma hili tunaangalia nini maana hasa ya kuwa mhitimu wa kozi hii. Uwezo wa dhana hizi rahisi ambazo umekuwa ukijifunza, kubadilisha maisha yako. Uwezekano mkubwa wa fursa zilizo wazi kabisa mbeleni, kwa ajili ya maisha yako ya baadaye. Huenda usione chochote ni tofauti, lakini umebadilika.
Sasa ndani yako unayo DNA ya kuwasha uamsho wa kweli. Popote duniani. Wakati wowote. Fuatilia yale ambayo umejifunza kwa moyo wako wote na hakika uamsho utazuka. Siku za kusisimua zaidi maishani mwako zingali punde tu mbeleni.
Mhariri,
Amefichwa katika Kristo |
These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST
Mabomu Yatembeayo
Revival Keys > Juma la 8 > Malengo
| Jina: |
|
|
Imesainiwa na: |
| Tarehe: |
|
 |
Kwa uchunguzi wa Biblia wa juma hili, nataka ujikite katika Mathayo 10:1-42. Haya ni maagizo ambayo Yesu aliwapa wanafunzi Wake kabla hajawatuma. Ni marefu kidogo, kwa hivyo utaweza tu kupitia vidokezo, lakini yanastahili juhudi husika. Kumbuka, maneno haya hayakuwa kwa ajili yao tu, bali pia kwa ajili ya kila mtendakazi wa baadaye... |
 |
Kote katika masomo haya, nimezungumza mara kwa mara kuhusu hitaji la kuwa Wakala halisi wa Uamsho. Juma hili tutakuwa tukichimba zaidi maana yake. Mwombe Mungu akupe hata kipimo zaidi cha Roho Wake kadiri unavyofanyia kazi jambo hili. |
 |
Anza kukariri Isaya 49:6. Ni ndefu kidogo, lakini ni moja ya aya nzuri zaidi katika Biblia. Na hakika inastahili juhudi hiyo! Unapoifanyia kazi, mwombe Mungu akuze imani yako, na akusaidie kukumbatia kikamilifu kile ambacho inaahadi. |
 |
Nyenzo ya Ziada katika juma hili ni Marudio mafupi juu ya Uanafunzi. Tumia muda mchache kufanya tathmini aminifu ya maisha yako. Je, kuna mapungufu katika kutembea kwako na Mungu? Unaweza kufanya nini ili kuyarekebisha? |
 |
Unajua mazoezi. Omba, omba, omba—kwa ajili ya uamsho halisi. Uamsho kwako mwenyewe. Uamsho kwa timu yako. Uamsho kwa kanisa lako. Inaweza kuchukua muda hadi Mungu ashughulikie vikwazo, lakini inaweza kutokea—ukiamini. |
FAST
Mwaminifu, Aliye Tayari, Mtu wa Kiroho, Mwelekevu
Mabomu Yatembeayo
Revival Keys > Juma la 8 > Kuchunguza Maandiko
Mada: Mathayo 10:1-42
Muhtasari Mfupi:
Maoni/Dondoo:
Kanuni & Matumizi:
Wazo Kuu:
Mabomu Yatembeayo
Revival Keys > Juma la 8 > Mapendekezo ya Kivitendo
Mawakala wa Uamsho
Ikiwa umefanikiwa kufika hapa katika kozi yetu ya Funguo za Uamsho, uko tayari kuanza huduma yako kama wakala wa uamsho. Unajua hitaji letu la haraka la uamsho. Unajua masharti muhimu ya uamsho: kusoma kwa bidii, maombi ya dhati, utii thabiti, na huduma ya kujitoa. Nawe una nyenzo za kufanikisha mambo hayo. Una mkakati wa msingi wa kuibua uamsho kanisani mwako, na kutunza na kudumisha uzoefu huo. Nawe unajua nguvu ya timu thabiti za huduma ili kudumisha mwendo na hatimaye kubadilisha kanisa lako. Huenda usijisikie tofauti kiasi hicho, lakini umebadilika.
Katika mapendekezo ya kivitendo juma hili, tunataka kuangalia nini maana halisi ya kuwa wakala wa uamsho. Uwezekano ulio mbeleni kwa ajili ya maisha yako mapya. Nguvu ya mafunzo ambayo umepokea. Ili kufanya hivyo, tunataka kuanza kwa kuangalia aya yenye utata zaidi...
Uamuzi wa Kutatanisha
Nyakati fulani wahusika katika Biblia hufanya maamuzi yanayoonekana kuwa ya ajabu kwetu, kwa sababu hatuelewi hasa fikra zao. Zingatia uamuzi ambao Paulo aliufanya katika 2 Wakorintho 2:12-13. Katika ibara hii ya maandiko, tunamwona Paulo akiingia kwenye mji mpya: Troa. Na anaenda hapo kwa kusudi maalum: kulihubiri injili. Na anapofika, kitu fulani kinatokea: mlango unafunguliwa kwa ajili yake. Mlango ambao Biblia inaweka wazi kwamba Bwana alimfungulia Paulo. Ni dhahiri kwamba mji huo ulikuwa radhi kuupokea ujumbe wake. Watu walikuwa na shauku ya kupokea mafundisho yake. Ulikuwepo uwezekano wa mamia, huenda maelfu, kuja kwa Kristo!
Lakini Paulo anajikuta akisawazisha fursa hiyo kwa tatizo lingine linalomsibu. Paulo anataja jinsi ambavyo hakuwa na utulivu rohoni mwake, kwa sababu hakujua kilichokuwa kikimtokea Tito, rafiki na mshirika wake katika huduma. Kwa upande mmoja, angekaa Troa na kuwaleta wengi sana kwenye wokovu. Au angeweza kuyaacha yote, ili kujielekeza kwa mtu mmoja ambaye tayari amekabidhi maisha yake kwa Kristo. Kama ungekabiliwa na chaguzi hizo, ungeamua nini?
Wengi wangejikita kwenye mji husika. Lakini Paulo anasema aliondoka Troa, na kwenda Makedonia, bila shaka ili kumtafuta Tito! Aliacha fursa dhahiri kabisa ya kuongoa roho, ili kumfuatilia mtu mmoja. Kwa nini?
Dhana Kuhusu Mtu Muhimu
Tunaweza tusijue kamwe sababu halisi, lakini naamini inahusu zaidi mafunzo. Tito alikuwa ametumia miaka mingi akihudumu pamoja na Paulo, na Paulo alijua kwamba mafunzo yalikuwa yamemfanya Tito awe mwenye manufaa sana kwa kazi ya Kristo.
Bila shaka Paulo alikuwa amewekeza sana kwa Tito, akihawilisha kwake maarifa yenye thamani, ujuzi, maono. Wakati akimsifu Tito baadaye katika waraka wake kwa Wakorintho, Paulo angeweza kusema: “hivi hatukuenenda katika roho ileile? Je, hatukutembea katika hatua zilezile? (2 Wakorintho 12:18). Kama vile alivyoandika kumhusu Timotheo, Paulo angeweza kumtegemea Tito ili kuwaleta wale aliowafundisha ili waingie “katika ukumbusho wa njia zangu zilizo katika Kristo, kama nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa” (1 Wakorintho 4:17). Kimsingi Paulo alikuwa amejinakilisha mwenyewe katika Tito. Na katika Timotheo. Na katika wengine.
Je, kielekezo cha huduma ya Paulo kilikuwa nini? Ukichunguza mbinu yake halisi, unaona alikuwa akienda kwenye mji fulani, akalikusanya kundi pamoja, akaligeuza kanisa hilo kuwa kituo cha mafunzo, na kuanza kuwekeza katika maisha ya watu. Punde uamsho ulikuwa ukitokea, na Injili ilikuwa ikipuka katika eneo jirani. Tazama Matendo 19:8-10. Ndicho kile hasa kilichotokea popote alipoenda Paulo. Na bila shaka watendakazi ambao Paulo aliwafundisha waliifuata mbinu hiyohiyo pia.
Jambo ambalo huelezea kwa nini Paulo alimchagua Tito badala ya Troa. Tito hakuwa mtu mmoja tu, bali ufunguo wa kufungulia mji mzima, eneo zima. Tito alikuwa muhimu zaidi kuliko Troa, kwa sababu kama Paulo kwa namna fulani angefanikiwa kumrejesha katika huduma, wangeweza kufikia miji miwili, maeneo mawili. Paulo hakuwa tu akimtazama mtu mmoja, alikuwa akitazama umati wa watu wasiohesabika ambao huyo mtu mmoja angeweza kuwafikia.
Mafunzo ndiyo yalimfanya Tito awe wa thamani sana. Alibadilika kuwa mtu muhimu sana. Aligeuka kuwa wakala wa uamsho.
Njozi ya Ulimwengu
Mafunzo ambayo umepokea hii miezi michache iliyopita yanakupa thamani ileile. Iwapo uamsho ukiendelea ukiwaka moyoni mwako, utapata shuhuda za kuwasimulia wengine. Na hilo litavuta watu binafsi, wenye njaa ya kukua. Nawe unajua jinsi ya kuwasaidia. Wakati fulani, unaweza kuunda timu, na kuanza kuwafunza kwa utaratibu: katika kukariri, uanafunzi, na uamsho. Na punde uamsho utakuwa ukiangaza sana katika kundi hilo jipya muhimu. Bila shaka, utamiminika na kusambaa ndani ya kanisa lako. Timu nyingi zaidi zitaundwa. Na kadiri kanisa lako linavyopata huisho—utamiminika na kusambaa katika jamii yako. Punde utakuwa mmoja miongoni mwa wengi, wanaofanya kazi na kumsifu Mungu pamoja.
Baada ya muda, utaenea kwenye makanisa ya eneo husika. Baadhi ya wale unaowafunza watahamia maeneo mengine, na wataweza kuibua uamsho katika makanisa hayo mapya. Labda utaitwa kuhama kwa sababu moja au nyingine, na kupata fursa ya kuweza kuanza mchakato wote huu tena, kwa mara nyingine, mahali pengine. Kutoka mahali hadi mahali, uamsho utasambaa. Hilo linaweza kutokea.
Kwa nini? Kwa sababu wewe ndiye huyo mwanaume au mwanamke muhimu ambaye Mungu anaweza kumtumia ili kufungua miji mizima, maeneo yote. Kwa sababu umeandaliwa na kuwezeshwa ili kuishi kama wakala wa uamsho.
Kwenye FAST, tunaamini njozi ya ulimwengu ni kuuona ulimwengu kupitia mtu mmoja. Kuuona uwezo wa mtu mmoja kuongezeka na kuwa elfu (Isaya 60:22). Kwa kuona kwamba Mungu amemwita kila mmoja wetu, ili awe wokovu Wake “hadi mwisho wa dunia.” (Isaya 49:6) Hivyo ndivyo tunakuona wewe...
Kweli, hakuna ukomo wa kile ambacho Mungu anaweza kufanya kupitia mtu mmoja aliye radhi kumpatia Roho Mtakatifu nafasi ya kufanya kazi kupitia maisha yake. Kupitia mtu mmoja aliye tayari kuwa wakala wa uamsho.
Kumbuka: Kwa maelezo zaidi kuhusu kuwa kiongozi wa kiroho, na kukuza zaidi nadhari zako zote za kiroho, angalia miongozo yetu ya kujifunza iitwayo Mitambo ya Maadili, kwa kututembelea katika WWW.FAST.ST.
Mabomu Yatembeayo
Revival Keys > Juma la 8 > Nyenzo za Ziada
Marudio Kuhusu Uanafunzi
Kuwa wakala wa uamsho kunahitaji msingi wa maisha sawia ya uanafunzi. Hii hapa orodha hakiki ya stadi 28 za msingi wa uanafunzi zinazopendekezwa. Itumie ili kuhakikisha kwamba hakuna vipande vinavyokosekana katika maisha yako ya kiroho:
Nimemwalika Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wangu binafsi.
Nimeazimu kulifanya zoezi la kukariri liwe sehemu endelevu ya maisha yangu.
Nimeweka kiwango cha chini cha kasi ya idadi aya za kujifunza kila juma.
Nina mpango wa marudio uliopangiliwa vyema ili kuhakikisha kwamba nahifadhi aya nilizokariri.
Nakutana na mshirika au kikundi kwa muda maalumu kwa ajili ya uwajibikaji wa kukariri.
Najifunza Biblia kila siku, nikitafuta kanuni zinazozungumza nami.
Mara kwa mara nafungamanisha Neno kwenye maisha yangu kupitia miradi binafsi.
Naweza kufanya zoezi la kujifunza Biblia kwa udukizi wa ibara ya maandiko yenye changamoto.
Natunza shajara amilifu ya maombi na kuomba kwayo kwa uaminifu.
Naunganisha ahadi mahususi za Biblia na mahitaji ya maombi yangu binafsi.
Narekodi tarehe ninazoombea mahitaji yangu, na jinsi ninavyomwona Mungu akitenda kazi.
Najua jinsi ya kuomba kimazungumzo katika kikundi.
Nadumu kutumia Maandiko kwa bidii katika maisha yangu ya maombi, na kusikiliza sauti ya Mungu.
Natumia orodha kuu ya utendaji ili kufuatilia mambo yote ninayohitaji kufanya.
Natengeneza orodha ya mambo ya kufanya kama sehemu ya ibada zangu za kila siku na kumkabidhi Mungu.
Nimetenga nyakati za mara kwa mara kukagua miradi, mipango, vipaumbele, na madhumuni yangu.
Najua jinsi ya kutumia maswali ili kuwahimiza wengine kwenye utii wa kina zaidi.
Nimeandika ushuhuda wangu binafsi na naweza kuusimulia kirahisi.
Naweza kueleza injili kwa mtu mwingine kwa kutumia lugha rahisi na iliyo wazi.
Najua vipengele saba vya huduma madhubuti ya kuwafikia watu.
Ninao ujuzi wa msingi unaohitajika ili kumsaidia muumini mwingine akue kiroho.
Naamini kwamba mafunzo kupitia timu huongeza zaidi ukuaji wa kiroho.
Naliona ongezeko la kiroho kama mpango wa Mungu wa uinjilisti wa ulimwengu.
Naamini uamsho ndilo hitaji letu kuu, na naliombea kila siku.
Najua jinsi ya kutafuta, kuchochea na kutunza uamsho.
Nimeazimu kwa dhati kuboresha maisha yangu kupitia elimu endelevu.
Mimi ni sehemu ya timu ya huduma iliyoazimu kutafuta uamsho.
Mimi binafsi nimedhamiria kuishi kama wakala wa uamsho kanisani mwangu.