Kukoleza Moto
Revival Keys > Juma la 4 > Dokezo
 |
|
Dokezo:
Je, uko tayari kwa ajili ya utafiti mwingine ukupao changamoto? Natumaini hivyo, kwa sababu juma hili tutazungumzia kukoleza moto wa uamsho.
Hivi umewahi kumwona mtu akijaribu kuuwasha moto wa kambi? Anakusanya rundo la vijiti na nyasi, kisha anawasha kiberiti. Mwale wa moto huanza ukiwa mdogo, na hafifu. Lakini ukiupuliza taratibu, huwaka moto mkali zaidi na kuanza kusambaa. Punde unaurushia magogo, na moto unawaka sana. Hicho nchicho tunazungumzia leo...
Masomo ya Biblia ambayo tumekuwa tukifanya ni vile vipande vidogo vya kuwashia moto. Na maombi ndiyo yanawasha kiberiti. Juma hili tutaangalia jinsi ambavyo mausia hukoleza mwale wa moto. Je, uko tayari?
Mhariri,
Amefichwa katika Kristo |
These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST
Kukoleza Moto
Revival Keys > Juma la 4 > Malengo
| Jina: |
|
|
Imesainiwa na: |
| Tarehe: |
|
 |
Uchunguzi wa Biblia wa juma hili ni Matendo 11:19-26. Inaangazia moja ya wahusika wa Biblia ninaowapenda sana, ambaye huduma yake ilisaidia kujenga moja ya vituo imara zaidi vya mafunzo katika Agano Jipya. Uamsho, kwa kweli. Tumia muda kuchimba ndani zaidi katika ibara hii ya maandiko na ujaribu kutambua siri ya mafanikio yake. |
 |
Soma habari iliyo mbeleni yenye kichwa kisemacho Mausia yenye Faraja. Unapofanya hivi, tafakari juu ya kushiriki kwako katika timu yako. Je, unawatia moyo, unawapa changamoto, na kuwaunga mkono wengine ili wafanikishe malengo yao bora zaidi? Je, unaonesha kilelezo hicho, kwa kutoa kilicho bora zaidi? |
 |
Aya ya kukariri wa juma hili ni Waebrania 3:13-14. Inaelezea hatari za kupuuza ushirika wa kibiblia, na baraka iliyoahidiwa inayoambatana nayo. Kuwa tayari kunukuu aya hii kwenye mkutano wako unaofuata wa timu, pamoja na aya zako zingine zote kufikia sasa. Kumbuka, daima fanya marudio ya marejeleo-aya-marejeleo. |
 |
Iwapo tunakusudia kwa dhati kufanya uamsho, tutalazimika kuamua kwa dhati kuondoa dhambi inayojulikana. Nyenzo ya ziada juma hili zinabainisha mkakati rahisi wa Ushindi dhidi ya Dhambi. Na inafanya kazi... |
 |
Endeleza umakini wako wa maombi kwenye uamsho. Juma hili, jaribu kufanya utaratibu wa kumwombea kila mshiriki wa timu yako kwa jina. Mwombe Mungu atende kazi kwa nguvu ndani ya kila mmoja wao, akiwapa shauku kubwa ya utii. Na dhamira kubwa zaidi ya kutafuta uamsho. |
FAST
Kujikita Kutimiza Majukumu Mahususi
Kukoleza Moto
Revival Keys > Juma la 4 > Kuchunguza Maandiko
Mada: Matendo 11:19-26
Muhtasari Mfupi:
Maoni/Dondoo:
Kanuni & Matumizi:
Wazo Kuu:
Kukoleza Moto
Revival Keys > Juma la 4 > Mapendekezo ya Kivitendo
Mausia yenye Faraja
Uamsho wenye nguvu daima hujikita kwenye uanafunzi halisi. Lakini uanafunzi halisi huhitaji azma ya dhati. Kudumisha uaminifu katika maombi, kujifunza Biblia, au kukariri ya Maandiko ni ngumu. Utii thabiti linaweza kuwa suala linalohitaji pambano. Kujaribu kushuhudia ni ngumu. Lakini Biblia inatupatia suluhisho: "mwonyane kila siku ... ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi" (Waebrania 3:13). Tunahitaji mausia. Changamoto na faraja ya Wakristo wenzetu ili kutusaidia kusonga mbele. Na hilo ni muhimu, kwa kuwa tu “tunafanywa washirika wa Kristo” iwapo tukidumu kuwa “imara hadi mwisho" (Waebrania 3:14).
Mahali bora pa kupata aina hii ya mausia ni katika timu ndogo ya waumini wenye azma ya dhati. Kikundi ambacho kila mhusika anashiriki lengo lilelile la uanafunzi wa kina zaidi. Kikundi ambacho kila mtu yuko tayari kusaidiana na kutiana moyo. Kundi lililokusudia kwa dhati kuishi kwa ajili ya Kristo. Kikundi kilichodhamiria kutafuta uamsho. Katika aya zinazofuata, tutabainisha funguo chache za kuunda kikundi cha aina hii.
Sisitiza Utii
Hatua ya kwanza katika mausia yenye faraja ni kumhamasisha kila mshiriki wa kikundi aone umuhimu wa utii binafsi kwa Mungu. Utii siyo tu ufunguo wa kuurithi uzima wa milele (Ufunuo 22:14), pia ni ufunguo wa karibu kila eneo lingine la uanafunzi. Ni ufunguo wa kulielewa Neno la Mungu (Yohana 7:17). Ufunguo wa nguvu katika maombi (Zaburi 66:18). Na ufunguo wa kushuhudia kwa ufanisi, pia (1 Wathesalonike 1:5). Na huwezi kuepuka umuhimu wa utii katika suala la uamsho. Biblia huweka wazi: Mungu huwakirimia “Roho Mtakatifu ... wale tu wanaomtii" (Matendo 5:32).
Kivitendo, hii mara nyingi hujitokeza katika kipindi cha uwajibikaji cha mikutano ya timu yako. Je, una nia ya dhati kuangalia malengo ya kila mtu ili kuhakikisha yamekamilika? Au sehemu hii ya mkutano imepunguzwa. Je, kuna matarajio halisi ya kazi zitazokamilishwa? Au kuna vicheko vya aibu kuhusu kuruka vitu fulani vichache? Iwapo kazi fulani itathibitika kuwa ngumu, hivi kuna mawazo ya kutatua tatizo—yaliyoazimu kutambua kikwazo na kutafuta njia fulani ya kukiondoa? Je, ugumu wa mwanachama mmoja unakuwa mzigo wa kikundi kizima, au kila mtu anaachwa kuzama au kuogelea peke yake?
Haya siyo maswali rahisi. Na ikizingatiwa kwamba, si kila mtu atataka aina hii ya ushiriki. Lakini uhalisia ni kwamba, Wakristo wengi hawataweza kamwe kufikia uwezo wao kamili, bila changamoto dhahiri, msaada mkubwa, na uwajibikaji halisi. Kwa ufupi, mausia ni muhimu sana. Na wale wanaotamani uamsho watavutwa kwenye timu kama hii.
Umakini Kuhusu Matumizi
Pamoja na kukuza kipindi thabiti cha uwajibikaji katika timu yako, ni muhimu pia kwa timu yako kukuza mtazamo wa matumizi. Baada ya miaka mingi, nikifanya kazi na vikundi vingi, nimeshawishika kwamba matumizi binafsi ndicho kitu pekee ambacho asili ya mwanadamu hutafuta sana kuepuka. Hata hivyo ni muhimu sana kwa ajili ya badiliko halisi. Ikiwa timu yako inataka kukua kweli, kila mwanatimu yako lazima aamue kuishinda tabia hii.
Matumizi huwezeshwa kwa uamuzi rahisi wa kujitoa kwa dhati kutenda kulingana na Neno la Mungu, na kulitekeleza binafsi. Ni azma ya kuwa "mtendaji wa neno", na wala si msikiaji tu (Yakobo 1:22). Na ingawa mahali pazuri pa kufanyia mazoezi utekelezaji ni katika utulivu na faragha ya ibada zetu binafsi, bila shaka unaweza kuhimiza utekelezaji katika timu.
Labda rafiki fulani atakushirikisha jambo fulani lililozungumza naye wakati akiichunguza Biblia, katika aya ya kukariri, au kupitia jambo fulani katika mapendekezo haya ya kivitendo. Au anaweza kuonesha tu shauku ya kukua katika eneo fulani, au kufanikisha lengo fulani. "Nia njema" kama hizo zinaweza kuibuka wakati wowote—kwa hiyo kuwa macho!
Unaweza kumsaidia mtu fulani abadilishe "uwezekano" wa utekelezaji kama huu, kuwa mpango halisi wa utendaji kwa kuuliza maswali rahisi. Kaa karibu na watu wenye ujuzi wa kuuliza maswali kama haya na jifunze kuyauliza mwenyewe:
■ Je, una azma ya dhati kufanya hivyo?
■ Hivi hiyo ingeonekanaje, kwa namna ya kivitendo?
■ Nini kinakuzuia kufanya hivyo?
■ Je, hilo lingehitaji hatua gani za utendaji?
■ Nini unachoweza kufanya juma hili ili kuanza?
■ Je, kuna mtu yeyote mwenye maarifa kuhusu jinsi ya kufanya hili litokee?
■ Je, kuna njia fulani ninayoweza kukusaidia kwa hilo?
■ Je, hili ni jambo ambalo timu yetu inaweza kulifanyia kazi pamoja?
■ Je, tuko radhi kujitolea kufanya hili?
Rafiki fulani akijitolea kwenye mpango wa utendaji: andika, na uiongeze kwenye shajara yako ya maombi ili uweze kumwombea. Na kisha fuatilia. Uliza ilikuwaje mlipokutana tena. Mausia hutusaidia kushikilia miguu yetu motoni kwa kutushika tunapozungumza kwa ujumla, yakituita kwenye hatua mahususi za utekelezaji, na kisha kututia moyo njiani. Ndivyo Wakristo wanavyokua katika utimilifu wa Kristo (Waefeso 4:15).
Uwajibikaji hufanya kazi tu wakati kunapokuwepo motisha thabiti ya pamoja. Nia ya kuwa halisi katika kutembea kwetu na Mungu, pamoja. Shauku ya kusaidiana ili kuwa yote tunayoweza kuwa. Mwombe Mungu aamshe aina hiyo ya motisha moyoni mwa kila mtu kwenye timu yako.
Mausia ya Biblia
Mausia ni ya kibiblia. Na kama waumini, lazima tuone umuhimu wa kupeana changamoto ikiwa tuna nia ya kuja kufikia uwezo wetu kamili katika Kristo. Katika Agano Jipya tunaona kielelezo bayana cha mausia. Barnaba, alipoenda Antiokia, “akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo. Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu” (Matendo 11:23). Vivyo hivyo, yeye na Paulo “waliwaonya” wanafunzi wapya huko Listra na Ikonia “waendelee katika ile imani” (Matendo 14:22). Na baadaye Paulo, akisafiri katika Makedonia yote, akawapa “maonyo mengi” (Matendo 20:2). Kwa waumini wa Thesalonike, Paulo aliandika: “tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu” na mweze “kuzidi sana" (I Wathesalonike 4:1).
Kwa namna ya kusikitisha, ni Wakristo wachache wanaothamini umuhimu wa mausia leo. Tunapenda kujifunza, kuzungumzia hilo, au hata kubishana juu ya Maandiko—lakini tunapata shida kulifanya Neno la Mungu lilete badiliko maishani mwetu binafsi. Na wala hatufanyi vizuri sana katika kuwatia moyo wengine ili pia wayatumie Maandiko kivitendo. Matokeo yake ni kwamba kunaenea hali ya kutokomaa kiroho.
Ili kurekebisha hili, ni lazima tugundue upya sanaa ya upole ya mausia, na tuungane pamoja na waumini wenzetu ambao wana nia ya dhati kuimarisha mahusiano yao ya kutembea na Mungu. Jiunge uwe sehemu ya timu kama hii, ndipo utakuwa na uhakika wa kukua kiroho. Na hiyo inaweza tu kusababisha uamsho.
Kumbuka: Kwa taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kukua katika utii binafsi, na kuongozwa zaidi na Roho, angalia miongozo yetu ya masomo ya Kuingia Kazini, kwa kututembelea katika WWW.FAST.ST.
Kukoleza Moto
Revival Keys > Juma la 4 > Nyenzo za Ziada
Ushindi dhidi ya Dhambi
Biblia inafundisha wazi kwamba kuna nguvu ya ushindi katika Injili. Lakini linapokuja suala la mambo ya msingi, huwa hatujui jinsi ya kuyapata. Ufunguo mmojawapo ni kuelewa tu kwamba Injili inayotuokoa mwanzoni, ndiyo hututia nguvu kila wakati. “Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika Yeye” (Wakolosai 2:6). Kwa maneno mengine, Dondoo za Biblia zinazotuwezesha kumpokea Kristo, ndizo hutupatia ushindi wakati wa jaribu. Zingatia dondoo hizi:
Kiri: Kiri hali yetu ya kutoweza kufanya mema. Tambua tatizo la dhambi. Kwamba imejikita katika asili yetu. Kwamba tuko katika hali ya kukata tamaa. Kwamba bila msaada, hatuna nguvu.
Amini: Amini kwamba Kristo alilipa adhabu tunayostahili. Na matokeo yake ni kwamba tunaweza kupata msamaha kamili na ondoleo la dhambi. Kwamba damu ya Kristo hutuweka katika uhusiano mpya na Mungu, tukiwa na fursa kamili ya kupata neema Yake.
Dai: Dai uwezo wa Roho Mtakatifu. Kila kitu tunachohitaji ili tuishi kwa haki kimo ndani ya uwezo wetu, hivi sasa. Nguvu iliyopo haina ukomo. Tunahitaji tu kuishikilia kwa imani.
Kwa hiyo unafanya nini unaposhawishiwa na tamaa fulani ya kutenda mabaya? Igeukie Injili. Angaza maombi kwenda mbinguni kwa mpangilio huu. Kwanza KIRI: "Bwana, unajua navutwa kwenye hili. Mimi ni dhaifu. Siwezi kupinga hili peke yangu." Kisha AMINI: "Asante kwa ajili ya Yesu, aliyekufa msalabani. Nasihi damu Yake—nipokee." Na mwisho DAI: "Tafadhali, nipe nguvu ya kushinda. Nikirimie uwezo Wako, sasa hivi." Kisha kwa imani geuka.
Wakati mwingine ushindi ni rahisi. Jaribu huvunjika nasi tunabaki huru. Lakini nyakati zingine, tunayumba, na kuangalia nyuma. Tufanye nini basi? Tuma sala nyingine: "Bwana, siwezi kufanya hivi bila msaada. Nasihi kwa damu ya Kristo. Nami nashikilia nguvu Zako, sasa." Kisha geuka tena. Kulingana na nguvu ya jaribu, inaweza kuchukua awamu zingine kadhaa. Lakini ilimradi tu unang'ang'ania injili, huwezi kushindwa. Injili haishindwi kamwe.