Kuamshwa Kiroho
Revival Keys > Juma la 1 > Dokezo
 |
|
Memo:
Unapotazama kile kinachotokea katika ulimwengu wetu wa leo, huwezi kujizuia kuhisi kwamba mambo yanazidi kuporomoka kwenda nje ya udhibiti. Kwamba sote tunaserereka kuelekea kwenye zahama fulani inayokaribia. Jambo zito linaonekana kuwashikilia watu kila mahali. Na haya yote huelekea kwenye kurudi upesi kwa Kristo!
Ikiwa hilo linakuelezea wewe, basi pengine pia unahisi shauku ya kupanda juu zaidi katika kutembea kwako na Mungu. Kukabidhi maisha yako kikamilifu zaidi kwenye kusudi la Kristo. Na kuwasaidia wengine kukua kiroho pia. Unachotamani hasa ni uamsho.
Na hiyo ndiyo maana hasa ya masomo haya ya Funguo za Uamsho. Katika majuma yajayo, tutakupa ujuzi na nyenzo unazohitaji ili kuwa wakala wa uamsho. Uamsho miongoni mwetu ndilo hitaji kuu na la haraka zaidi katika mahitaji yetu yote. Na uamsho mkubwa unakuja. Jitayarishe!
Mhariri,
Amefichwa katika Kristo |
These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST
Kuamshwa Kiroho
Revival Keys > Juma la 1 > Malengo
| Jina: |
|
|
Imesainiwa na: |
| Tarehe: |
|
 |
Uchunguzi wako wa kwanza wa Biblia ni II Wafalme 7:3-9. Kifungu hiki ni tukio la kuvutia kutoka Agano la Kale linaloonesha baraka zinazopatikana kwetu kupitia uamsho, baraka ambazo kwa namna ya kusikitisha mara nyingi tunazikosa. Omba uongozi wa Mungu kadiri unapojifunza, chunguza kifungu hiki cha maandiko kwa makini, kisha ujaze mwongozo wa kujifunza wa juma hili kwa ubora kadiri uwezavyo. |
 |
Soma mapendekezo ya kivitendo mwishoni mwa kijitabu hiki yenye kichwa cha habari kisemacho Masharti ya Uamsho. Jiandae kuyajadili kwa kina katika mkutano unaofuata wa timu. |
 |
Aya yako ya kwanza ya kukariri ni Waefeso 5:14. Ikiwa umemaliza kozi zingine za FAST hapo awali, tumia muda fulani wa ziada juma hili kufanya marudio ya aya zako zilizopita. Iwapo hufahamu kanuni za msingi za kukariri Maandiko, tafadhali fanya Kozi yetu Fupi inayohusu kukariri Biblia katika WWW.FAST.ST/CC. Unaweza fanya hili! |
 |
Durusu nyenzo ya ziada yenye kichwa habari kisemacho Ahadi ya Wakala. Ikiwa tunakusudia kwa dhati kupata uamsho wa kweli, itahitaji azma binafsi. Je, uko tayari kuingia kikamilifu? |
 |
Tumia muda fulani maalum juma hili ukiomba kwamba Mungu amguse kila mwanatimu yako ili apate utambuzi wa kina ya hitaji letu la uamsho. Na kwamba kila mmoja aazimu kuutafuta kwa bidii katika majuma yajayo! |
FAST
Kumtafuta Mwokozi Leo
Kuamshwa Kiroho
Revival Keys > Juma la 1 > Ibara ya Kuchunguza
Mada: II Wafalme 7:3-9
Muhtasari Mfupi:
Maoni/Dondoo:
Kanuni & Matumizi:
Wazo Kuu:
Kuamshwa Kiroho
Revival Keys > Juma la 1 > Mapendekezo ya Kivitendo
Masharti ya Uamsho
Uamsho miongoni mwetu ndilo hitaji kuu na la haraka zaidi kati ya mahitaji yetu yote. Kuutafuta huo inapaswa iwe kazi yetu ya kwanza. Kukariri Biblia kunaweza kuwa cheche ambayo hutuhuisha kiroho. Na maisha madhubuti ya uanafunzi yanaweza kuwa msingi wenye nguvu kwa ajili ya maisha yaliyojaa Roho. Lakini ikiwa tutasonga mbele ili kuwa wenye ufanisi zaidi katika huduma, tutahitaji jambo fulani zaidi. Tutahitaji aina ya nguvu inayokuja wakati wa uamsho.
Uamsho utahuisha nguvu zetu za kiroho, utambuzi wetu juu ya wajibu, usabilifu (kujikabidhi) wetu kwa Kristo, na imani yetu katika makusudi ya Mungu. Itaangazia mwenendo wetu wa kuichunguza Biblia, na kuchochea maombi yetu. Uamsho huibua usadikisho juu ya dhambi, toba ya kweli, na ari ya kutii. Na hutupa moyo wa huduma, ndani na nje ya kanisa. Kwa ufupi, uamsho huleta uhai katika kila kipengele cha uzoefu wa Kikristo wa mtu.
Ikiwa wewe binafsi hujawahi kupata uzoefu wa kumwagwa Roho Mtakatifu, unaelekea kwenye tukio la kusisimua katika majuma yajayo. Tunaenda kuchunguza hasa jinsi ya kutafuta uamsho, kuuchochea, na kisha kuulinda uzoefu unapokuja. Jitayarishe!
Mambo Manne Muhimu
Kabla ya kufika mbali sana katika somo letu la uamsho, ni muhimu kujua kwamba maandalizi makini yanahitajika. Hususan, kuna masharti nne:
Kusoma kwa Bidii
Hatua za kuelekea uamsho kwa kawaida huanza na uzoefu wa kina zaidi katika Neno. Kwa kukusudia kwa dhati zaidi kuyaingiza Maandiko moyoni. Hii ni pamoja na kujifunza jinsi ya kutambua kanuni za kibiblia na kuzigeuza kuwa miradi ya kivitendo. Huja kama matokeo ya kujifunza kuingia katika mawasiliano halisi, ya kisuhuba pamoja na Mwalimu Mkuu kila asubuhi.
Kadiri ustadi wetu katika kutafakari na matumizi unapokua, tunajifunza kuitambua sauti ya Roho wa Mungu kwa uwazi zaidi. Shani za Biblia huanza kufunguka. Tunajikwaa kwenye mirija ya ile kweli ambayo kamwe haikuonekana au kuthaminiwa hapo awali. Kama wale watu wawili waliokuwa njiani kuelekea Emau, mioyo yetu huanza kuchoma ndani yetu. Hii ni hatua ya kwanza kuelekea katika uamsho.
Maombi ya Dhati
Kusoma kwa bidii huvuvia hatua inayofuata katika mchakato wa uamsho—maombi ya dhati. Kadiri mapenzi ya Mungu yanapodhihirika zaidi, tunaanza kutambua hitaji letu, na kutoamini kwetu. Nia na mitazamo hufunuliwa. Kujichunguza binafsi kwa uaminifu husababisha kiburi kushushwa. Usadikisho huamka moyoni na tunahisi kushurutishwa kuingia katika uwepo hasa wa Mungu, kwa ajili ya msamaha, na uwezo wa kubadilika.
Tunaanza kujifunza jinsi ya kuawana na Mungu, na kushikilia nguvu za kiungu kupitia imani stahimilivu. Na kadiri tunavyoonja ushindi halisi, ndivyo tunavyotamani hata kiwango kikubwa zaidi cha Roho. Toba kama hii, daima ni sehemu muhimu sana ya maandalizi. Uamsho hauji kamwe, isipokuwa katika kujibu maombi.
Utii wa Dhati
Kadiri usabilifu wetu kwa Kristo unapoongezeka, azma yetu ya utii itakua pamoja nao. Tunadhamiria kushughulikia vyema zaidi suala la kutunza muda wetu. Tunatafuta maana ya kusudi dhahiri zaidi, vipaumbele vilivyo wazi zaidi. Tunabadilisha ratiba yetu ili kuruhusu nafasi zaidi kwa ajili ya mapenzi ya Mungu maishani mwetu. Tunakuwa makini kufuatilia kila kazi tunayohitaji kufanya, na kuzitekeleza kwa uaminifu. Tunajitahidi kutoacha chochote bila kukamilisha.
Pia tunaanza kutafuta mausia na uwajibikaji kutoka kwa wengine wenye matamanio kama hayo. Na tunasonga mbele pamoja katika kutafuta mapenzi ya Mungu. Kilio chetu cha mioyo yenye nia moja kinakuwa, "Ungependa nifanye nini?" Na baada ya muda, Mungu anaanza kufunua mpango fulani.
Huduma ya Kujitoa Kafara
Kwa kawaida mpango huo unahusisha aina fulani ya huduma. Mkakati fulani wa kuanza kuwafikia wengine katika familia, kanisa, au jamii yetu. Wema wa Kristo, katika kutubariki sana, hutushurutisha kutafuta njia za kuwabariki wengine. Hatuwezi kuifungia kwetu wenyewe. Maisha yetu hujaa utume.
Na tunajiunga na wengine katika huduma, ili kujaribu mambo makubwa kuliko yale ambayo tungeweza kuyapata kwa uwezo wetu wenyewe. Tunatanua wigo nje ya eneo letu la starehe, na tunahisi kushurutishwa kujitoa kwa dhati ili kufanikisha mradi wetu. Katika kila changamoto, tunasukumwa kutafuta hata kiwango kikubwa zaidi cha nguvu na uwepo wa Mungu. Na Mungu hujibu maombi hayo. Hatimaye, maisha huongolewa kwa ajili ya ufalme.
Ni mbinu rahisi, lakini iliyojaribiwa na ya kweli kwa ajili ya uamsho: kusoma kwa bidii, maombi makini, utii wa dhati, na huduma ya kujitoa kafara. Njia ikitayarishwa, uamsho utakuja...
Siku ya Pentekoste
Hiki ndicho hasa kilichotokia katika Siku ya Pentekoste, ama sivyo? Walikuwa wamekaa siku 10 ghorofani, wakiyatafakari maneno ya Kristo, masomo aliyokuwa amewafundisha, Maandiko aliyokuwa amewafafanulia. Taratibu uelewa wao ukaanza kufunguka. Wakasadikishwa kwa kina juu ya mapungufu na kushindwa kwao, nao wakaanza kumtafuta Mungu kwa maungamo ya unyenyekevu, na kutubu kutoamini kwao. Kupitia maombi ya bidii, mioyo yao ililainishwa. Nao wakaazimu kufanya vizuri zaidi. Kuishi maisha ya uaminifu na uadilifu. Walijikabidhi kikamilifu zaidi kwenye kazi ya Kristo—maelekezo Yake wakati wa kuwaaga kwamba wapeleke habari njema katika ulimwengu uliopotea. Ukubwa wa kazi husika uliwalemea, na walitambua kwamba ni uwezo wa kiungu pekee ndio ungeweza kuifanya kazi hiyo ikamilike. Walimsihi Mungu awape ujasiri na uthabiti waliouhitaji. Na wote walipokuwa tayari, wanaume na wanawake hao ghorofani walihuishwa kwa nguvu za Mungu.
Hilo linaweza kutokea tena. Na kwa kweli, lazima litokee. Ufunuo unaelezea wakati mara tu kabla ya kurudi kwa Kristo ambapo Yohana anaona “malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye uwezo mwingi; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake” (Ufunuo 18:1). Ni tumaini lililojaa ahadi. Wakati wa nuru na nguvu kuu ya kiroho. Wakati wa uamsho, wa kuburudishwa kwa watu wa Mungu. Uamsho mkuu sana unaozunguka ulimwengu.
Ufunuo siyo mahali pekee ambapo uamsho huu umetabiriwa. Habakuki anabainisha wakati ambapo dunia “ilijaa maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yaifunikavyo bahari” (Habakuki 2:14). Isaya anatabiri wakati ambapo Mungu atawaambia watu Wake “ondoka, ukaangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa BWANA umekuzukia” (Isaya 60:1). Na kisha kuna ahadi hii katika kitabu cha Yoeli: "Tena itatokea kwamba nitamimina Roho Wangu juu ya wote wenye mwili" (Yoeli 2:28).
Aya hizi, na zingine nyingi, zote zinaelezea tukio kuu moja la mwisho la kumwagwa Roho Mtakatifu. Uamsho wa mwisho duniani. Na uko punde tu mbeleni kwa watu wa Mungu! Ndiyo maana lazima tujifunze jinsi ya kuwa wakala wa kweli wa uamsho...
Kumbuka: Kwa taarifa zaidi kuhusu uamsho wa mwisho duniani, na jinsi ambavyo Maandiko kutunza kumbukumbu ya Maandiko huweza kutusaidia kujitayarisha kwa ajili ya hilo, angalia kitabu chetu kinachoitwa Kwa Wakati Kama Huu, kwa kututembelea katika WWW.FAST.ST.
Kuamshwa Kiroho
Revival Keys > Juma la 1 > Nyenzo ya Ziada
Ahadi ya Wakala
Uamsho ndilo hitaji kuu na la haraka zaidi katika mahitaji yetu yote. Kuutafuta huo inapaswa iwe kazi yetu ya kwanza. Lakini uamsho siyo kwa ajili ya wazimiao moyo!
Ingawa unaweza kuja mara hiyo, na wakati hutarajii sana, kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba utakuja baada ya kudumu kumtafuta Mungu kwa muda fulani. Iwe ni kwa sababu Yeye anapima uaminifu wetu, badiliko fulani linahitaji kutokea mioyoni mwetu, au kitu kingine kabisa—ni muhimu sana kwamba tuazimu kutafuta uhuisho kwa ajili ya muda huo.
Moja ya njia bora zaidi za kudumisha umakini katika lengo hili ni kuandika ahadi ya kila siku na kuipitia kila asubuhi kwa muda ufupi mwanzoni mwa ibada zako—ili kupangilia upya azma yako. Ikiwa kusudi lako ni kuishi hasa kama wakala wa uamsho, zingatia kuweka Ahadi yetu ya Wakala, ahadi yako, kila asubuhi kwa kipindi cha kozi hii. Ni njozi yetu ya kile kinachomaanisha kuwa wakala halisi wa uamsho:
Naahidi kuishi leo kama wakala wa uamsho kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.
Wakala lazima ajikabidhi kwa Mfalme Yesu kila siku, Masihi aliyeahidiwa, Mwokozi, na Amiri Jeshi Mkuu.
Wakala lazima apokee maelekezo ya kila siku kupitia mawasiliano ya moja kwa moja na mbingu, na atekeleze kila kazi aliyopangiwa kwa ubora kadiri ya uwezo wake.
Wakala lazima akuze ushawishi wake kwa kuendelea kufanya maboresho ya kila nguvu za kimwili, kiakili na kiroho.
Wakala lazima aazimu kutafuta uamsho kwa uaminifu hadi dunia iangazwe utukufu wa Mungu.
Kuwa huru kusahihisha maneno kadiri yanavyohitajika ili kuyafanya yawe yako hasa. Kisha azimu kuweka upya ahadi yako kwa Mungu kila asubuhi—halafu angalia kile ambacho Mungu anafanya!