Maisha Yenye Malengo
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 9 > Dokezo
 |
|
Dokezo:
Umefikia somo la mwisho katika Mafunzo ya Msingi, na hii ni muhimu ilioje! Juma hili tunaangalia chanzo muhimu cha nguvu ambacho inayohitajika sana kwa kila kipengele cha uanafunzi ambacho tumejifunza kufikia sasa. Pia ni kiini cha kudumu kuwa mwaminifu katika uanafunzi wako binafsi katika miaka ijayo.
Kufikia sasa, hakika umegundua uanafunzi ni zaidi ya kujifunza tu mbinu chache za kukariri—ni mtindo wa maisha. Mungu anataka Neno Lake liwe nguvu hai katika kila eneo la uzoefu wetu wa Kikristo. Linapaswa kubadili fikra yetu, kuelekeza hatua zetu, na kuvuvia sala zetu. Hutukinga dhidi ya majaribu. Hutuandaa kwa ajili ya huduma. Na hutuwezesha ili kuwafanya wengine kuwa wanafunzi. Hufanya haya yote na zaidi!
Ikiwa umefurahia kujifunza stadi hizi, basi endelea kusonga mbele. Usigeuke nyuma! Itakuwa tamu zaidi ikiwa utaazimu kuendelea kusonga mbele katika jitihada zako za kuliishi Neno la Mungu. Siku baada ya siku, na kidogo kidogo, utazidi kujawa Roho Mtakatifu.
Mhariri,
Amefichwa katika Kristo |
These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST
Maisha Yenye Malengo
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 9 > Malengo
 |
Kamilisha Uchunguzi wa Biblia wenye kichwa kisemacho Maisha Yenye Malengo. Somo hili linaangazia siri ya uanafunzi wenye mafanikio. Kwa kweli, ni siri ya maisha yote ya Kikristo. Tunaomba kwamba nyenzo zilizomo katika somo hili ziwe kile hasa unachohitaji ili udumu kuwa mwaminifu katika kutembea kwako na Kristo katika miaka yote ijayo! |
 |
Ni vigumu kuamini, lakini tumefikia aya yetu ya mwisho. Nayo ni madhubuti: 2 Yohana 1:8. Tumia muda fulani kuhakikisha unafanya kile hasa ambacho aya hii inasema. Ni juma lako la mwisho. Weka lengo la kukariri aya zote tisa, kwa usahihi, na kuhitimisha kwa rejeleo! |
 |
Soma Mapendekezo ya Kutendea Kazi ya mwisho katika programu hii. Na tumia muda fulani kuombea nyenzo hizi kwa dhati. Je, Mungu anakuita ili utoe maisha yako kwa kusudi gani hasa? Hilo ndilo swali, ama sivyo? |
 |
Endelea kupitia upya vielelezo vyote ambavyo tumejifunza hadi sasa. Ikiwa bado hujafanya hivyo, hakikisha hili ndilo juma ambalo hatimaye utazimudu zote. |
 |
Tumia muda maalumu katika maombi juma hili ukimwomba Mungu akupe angalau mtu mmoja unayeweza kumsaidia aanze kukua kiroho. Chukua changamoto hiyo ya kujenga maisha ya wengine. |
Haijalishi unaanza vizuri kiasi gani
Bali namna gani unamaliza vizuri
Maisha Yenye Malengo
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 9 > Uchunguzi wa Biblia
Alipofika na kuiona neema ya Mungu, akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa makusudi ya moyo. Matendo 11:23
1. |
Unaweza kuandikaje muhtasari wa uelewa wa Paulo kuhusu kusudi lake maishani? Wakolosai 1:28-29
|
2. |
Je, Paulo aliwahimiza waumini wa awali waishi maisha yao kwa kusudi kiasi gani?
I Wakorintho 15:58
Wafilipi 1:27
Wakolosai 1:9-10
|
3. |
Nini chanzo cha nguvu cha kuishi maisha yaliyojaa kusudi? Zekaria 4:6
|
4. |
Kwa nini Roho Mtakatifu ni muhimu katika maisha ya Mkristo?
Yohana 15:26
II Wakorintho 3:18
|
5. |
Ni katika maeneo gani mahususi ya uanafunzi ambapo Roho Mtakatifu anaweza kutuwezesha na kututegemeza?
Waefeso 6:18
Yohana 14:26
Ezekieli 36:27
Matendo 1:8
Unaweza kusema Roho Mtakatifu ni muhimu kiasi gani katika maisha ya mwanafunzi? |
6. |
Ni tukio gani lilituwezesha kupokea Roho Mtakatifu maishani mwetu?
Matendo 2:22-24, 33
Wagalatia 3:13-14
|
7. |
Sehemu yetu ni ipi katika kumpokea Roho Mtakatifu?
Luka 11:13
Yakobo 1:6
Yeremia 29:13
|
8. |
Je, uko radhi kiasi gani sasa hivi kuutafuta kwa moyo wako wote, kwa imani, uwezo wa Roho Mtakatifu ili atimize kusudi kuu la Mungu kwako—maisha ya uanafunzi wa kweli kuanzia siku hii na kuendelea hadi Yesu atakapokuja? Kwa nini usiandike jibu lako liwe sala fupi kwa Mungu? |
Maisha Yenye Malengo
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 9 > Mapendekezo ya Kutendea Kazi
Katika majuma machache yaliyopita tumejifunza mambo mengi. Na bila shaka, kadiri ambavyo umefanyia kazi masomo haya, moyo wako umepata changamoto kwa wito wa uanafunzi wa kina zaidi. Yamkini umepata uzoefu wa thamani pamoja na Bwana wakati huu, na hakika utataka haya yaendelee. Swali, hata hivyo, ni kwamba utakuwa wapi mwaka mmoja kuanzia sasa? Au mitano au kumi, tukichulia kwamba Kristo bado hajarudi? Je, kujitoa kwako kuishi kwa ajili ya Kristo kutakuwa imara wakati huo, kama ilivyo sasa? Je, utakuwa na azma ileile ya dhati katika kumfuata Mungu?
Kuna nguvu moja tu inayoweza kutudumisha kuwa waaminifu katika kipindi chote cha maisha yetu—na hiyo ni nguvu ya Roho Mtakatifu. Ili kuendelea kikamilifu kama wanafunzi wa Yesu Kristo, ni lazima tuwe wanaume na wanawake waliojazwa Roho. Tunaomba aya hizi hapa chini zikupe ufahamu wa kina zaidi wa maana yake halisi.
Kujazwa Roho
Ufunguo wa kwanza wa maisha yaliyojazwa Roho ni kutambua kwamba Mungu huwawezesha watu waliojazwa kusudi maishani. Barnaba, ambaye mwenyewe alielezewa kuwa “amejaa Roho Mtakatifu,” aliwapa changamoto waumini wa Antiokia “kushikamana na Bwana” “kwa kusudi la moyo” (Matendo 11:23-24). Vivyo hivyo, Paulo aliwaombea waumini wa kwanza, kwamba “wajazwe maarifa ya mapenzi Yake”—maana alijua kwamba ndipo Mungu angewaimarisha kwa kuwapa “uwezo wote, kadiri ya uweza Wake mtukufu” (Wakolosai 1:9, 11). Jikabidhi kwenye kusudi la Mungu kwa ajili ya maisha yako, na ndipo utakuwa na hakika ya kutegemea nguvu Zake!
Kwa kweli, kujenga utambuzi huo wa kusudi unahitaji muda. Muda mrefu, peke yako pamoja na Mungu—kuawana ili kuyajua mapenzi Yake kwa ajili ya maisha yako. Huzidi kuimarika kadiri tunapotumia muda katika kujifunza Biblia, maombi, kumkabidhi Yeye mipango yetu kila siku, na kushiriki katika huduma binafsi. Mungu hatukirimii Roho Mtakatifu kimsingi kwa ajili ya kujifurahisha na kukua kwetu binafsi—ingawa hakika haya ni matokeo ya uwepo Wake maishani mwetu. Badala yake, Mungu ana shauku kuu sana ya kuuokoa ulimwengu, na kila mahali anawatafuta wanaume na wanawake walio tayari kuyatoa maisha yao kwa ajili ya kusudi hilo. Na anapoona dhamira hiyo ya kushiriki, basi hutupatia kwa shauku uwezo wowote unaohitajika. Kujazwa Roho ni kujazwa kusudi.
Kutafuta Ubora
Utume wa juu na mtakatifu huvuvia juhudi za dhati. Ili kutimiza lengo lolote kubwa, ni muhimu kutimiza kazi nyingi ndogondogo vizuri. Ambapo ni sawa na kusema tu kwamba ufunguo wa kufanikisha kusudi lako maishani kihalisi ni suala la tabia. Kwa sababu Danieli alikuwa “mwaminifu, wala haukuonekana upotofu wala kosa ndani yake,” ikawa dhahiri kwamba “roho bora ilikuwa ndani yake” (Danieli 6:3-4). Ili kufikia uwezo wako katika Kristo, azimu kuutafuta ubora katika uanafunzi wako binafsi—na Mungu atakubariki kwa kukukirimia Roho Wake hata zaidi.
Hii ina maana ya azma kwa ajili ya maombi makini na ya dhati zaidi. Usahihi na kina katika kusoma Biblia na kukariri maandiko. Bidii na uadilifu katika utii na matumizi yako ya muda. Na, kwa upande wa uinjilisti, kudumisha ujasiri na ari. Ili kupata uzoefu maridhawa wa Roho wa Mungu, azimu kutafuta ubora katika kila kipengele cha kutembea kwako na Mungu!
Kukua katika Huduma
Kadiri unapopata ujuzi na uzoefu katika kila eneo la uanafunzi, nguvu za Roho wa Mungu zitazidi kukaa juu yako ili kuleta mabadiliko maishani mwa wale wanaokuzunguka. Maisha yako ya maombi yatageuzwa kuwa huduma ya maombezi. Wakati wako katika Neno la Mungu utakuwa huduma ya kufundisha—katika mazingira rasmi na yasiyo rasmi. Uaminifu wa maisha yako, na ushindi unaoupata utakufungulia milango ya kushiriki katika huduma ya kuwausia wengine. Na uzoefu wako katika kueleza ushuhuda binafsi utakuwa huduma ya uinjilisti kwa watu wengi zaidi. Huduma, kwa kweli, ni mwendelezo tu wa maisha yetu binafsi ya kutembea pamoja na Mungu. Tunda la uaminifu ni uzoefu kamili zaidi katika uwepo na nguvu za Roho Mtakatifu—maisha ya kila siku yaliyojazwa Roho. Huu ndio uanafunzi halisi.
Sasa una ujuzi na zana muhimu unazohitaji ili kuleta mabadiliko chanya katika ulimwengu wako. Ni maombi yetu kwamba utachagua kudumu ukiwa
umejitoa kwa ajili ya mambo ambayo umejifunza katika Mafunzo ya Msingi kwa miaka ijayo.
Je, uko tayari kuchukua hatua inayofuata? Tafuta kozi yetu ya Funguo za Uamsho, hatua inayofuata katika Njia ya Uanafunzi. Jifunze jinsi ya kuwa mwanamume au mwanamke huyo muhimu ambaye Mungu anaweza kumtumia ili kuleta uamsho katika familia, kanisa, na jamii yako. Uamsho mkubwa unakuja. Uko tayari?
Maisha Yenye Malengo
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 9 > Orodha-hakiki ya Mwisho
Ili kukamilisha programu hii, tafadhali thibitisha kukamilika malengo yafuatayo:
Maandiko ya Kukariri
Yohana 17:3
Zaburi 143:8
Warumi 4:20
II Wakorintho 8:11
Mithali 4:13
Warumi 1:16
Mhubiri 4:9-10
Isaya 60:22
II Yohana 1:8
Uchunguzi wa Biblia
Weka tiki hapa ikiwa umefanya hatua zote tisa za Uchunguzi wa Biblia
Mapendekezo ya Kutendea Kazi
Weka tiki hapa ikiwa umesoma Mapendekezo ya Kutendea Kazi yote tisa
Vielelezo
Gurudumu la Mwanafunzi
Baiskeli ya Kesha la Asubuhi
Upinde wa Ahadi
Uma
Kanuni ya Kukariri Maandiko
Dondoo za Biblia
Gurudumu la Mwanafunzi Larejelewa
Hongera! Sasa umemaliza Mafunzo Msingi ya FAST! Tunaomba tukiamini kwamba Mungu amebariki sana juhudi zako za kuishi maisha ya uanafunzi wa kina! Na tunakuhimiza uendelee kusonga mbele katika siku zijazo!
Je, programu hii imekuwa baraka kwako? Kwa nini usitutumie dokezo fulani, na kutueleza jinsi ambavyo imeleta badiliko maishani mwako? Asante!