Vikosi vya Waumini
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 7 > Dokezo
 |
|
Dokezo:
Karibu kwenye somo la saba. Unakaribia mwisho wa programu hii. Inaendeleaje hadi sasa? Je, unaendelea kumudu aya zako? Tafiti za Biblia? Vielelezo? Azimu kuyafanya Maandiko yawe halisi zaidi maishani mwako. Hebu liruhusu Neno lisilobadilika lifanye kazi yake.
Somo hili linalofuata linaangalia moja ya dondoo kuu za kudumu kuwa mwaminifu katika maisha ya mtu kutembea na Mungu: kazi ya pamoja. Kuhudhuria kanisani na mikusanyiko mingine ya kidini kuna manufaa, lakini haitoshi! Tunahitaji kutiwa moyo na kuhimizwa ambako huweza kupatikana kwenye timu ndogo tu, iliyoshikamana kwa ukaribu zaidi. Na kadiri tunavyokaribia mwisho, ndivyo litakavyokuwa jambo la maana zaidi kwa watu wa Mungu kusonga mbele pamoja. Usijihatarishe kwenda peke yako!
Uamsho wa kiroho wakati mwingine huanza na mtu mmoja, lakini kwa nadra hudumu muda mrefu akiwa amejitenga. Asili yake ni kuenea kutoka mtu hadi mtu, hadi kanisa lako lote limewaka! Na kisha kutoka hapo, utatafuta kupenya katika jamii yako. Hakika, unaweza kutokea.
Mhariri,
Amefichwa katika Kristo |
These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST
Vikosi vya Waumini
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 7 > Malengo
 |
Kamilisha Uchunguzi wa Biblia unaoitwa Vikosi vya Waumini. Je, kwa sasa unapata faraja na mausia unayohitaji ili kuwa thabiti katika kutembea kwako na Mungu? Kama ndivyo, unaweza kufanya nini ili kuhakikisha unaendelea kupokea aina hii ya ushirika? Ikiwa sivyo, unaweza kufanya nini ili uanze kuupata? |
 |
Aya zako za kukariri juma hili ni Mhubiri 4:9-10. Neno “ole” linakudokeza nini? Je, unapaswa kufanya nini ili kuiepuka? Pia, jaribu kufanyia kazi aya zozote ambazo huenda umezikosa. Tunakaribia mwisho wa kozi hii—azimu kuhitimisha kwa kishindo. |
 |
Soma Mapendekezo ya Kutendea Kazi juu ya umuhimu wa kazi ya pamoja. Kuwa sehemu ya timu ni ufunguo muhimu wa uthabiti katika maisha ya Kikristo. Pia ni muhimu kwa ufanisi katika huduma! Hebu mawazo mbalimbali katika uchunguzi huu yakusaidie kupata uzoefu kamili zaidi wa manufaa ya kazi ya pamoja. |
 |
Kielelezo chako cha mwisho, kinaitwa Gurudumu la Mwanafunzi Larejelewa. Kielelezo hiki kinakusanya pamoja kila kitu ambacho umejifunza hadi sasa, kuwa picha moja rahisi kuchora. Unapofanya marudio ya vielelezo vyako vingine juma hili, tafakari jinsi kila kimoja kinavyoshabihi picha kubwa zaidi. Je, kila kitu kinaunganika pamoja akilini mwako? |
Timu huwa thabiti tu
Kadiri ya kiungo dhaifu zaidi kwenye mnyororo husika
Vikosi vya Waumini
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 7 > Uchunguzi wa Biblia
Na kikaenda naye kikosi cha watu ambao Mungu alikuwa ameigusa mioyo yao. I Samweli 10:26
1. |
Bainisha sehemu mbili ambapo Wakristo wanaweza kupata faraja, mafunzo, na ushirika:
Matendo 2:46
Matendo 5:42
Matendo 20:20
Kumbuka: Wakristo wengi wanatambua umuhimu wa kuhudhuria kanisa mara kwa mara, lakini kukutana pamoja katika vikosi vidogo pia ni muhimu! Ni bayana vyote viwili vilikuwa muhimu katika kanisa la awali.
|
2. |
Kwa nini kukutana katika vikosi vidogo ni muhimu sana?
Waebrania 3:13-14
Waebrania 10:24-25
Kumbuka: Kuna baraka nyingi zilizofungamana na mikusanyiko ya hadhara, lakini hitaji letu la mausia na uwajibikaji mara nyingi huwa bado haujatimizwa bila ushirika wa timu iliyoshikamana kwa ukaribu zaidi. |
3. |
Ni vipengele gani vya uanafunzi vinaweza kuimarishwa kwa kujihusisha katika vikundi vidogo?
Mathayo 18:19-20
Luka 24:32
Wafilipi 3:17
Wafilipi 1:14
|
4. |
Nani alitumia timu ndogo kama msingi wa huduma katika aya zifuatazo?
Marko 3:14
Matendo 20:4
|
5. |
Paulo anaelezeaje hitaji letu la kufanya kazi pamoja? Waefeso 4:15-16
|
6. |
Ni zipi baadhi ya sababu za ziada ambapo kwa ujumla huduma huendeshwa vyema na timu?
Mithali 15:22
Mhubiri 4:9-10
Warumi 12:6-8
II Wakorintho 8:14
Walawi 26:7-8
|
7. |
Tunapaswa kujisikiaje pale ambapo hatuwezi kukutana mara kwa mara na Wakristo wengine kwa ajili ya ushirika? I Wathesalonike 2:17
|
8. |
Je, uko radhi kiasi gani kujitoa sasa hivi kukutana na waumini wenzako ili kufanya kazi ya kuwa wanafunzi fanisi zaidi wa Yesu Kristo? Kwa nini usiandike jibu lako liwe sala fupi kwa Mungu? |
Vikosi vya Waumini
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 7 > Mapendekezo ya Kutendea Kazi
Kama umekuwa mwaminifu katika kukamilisha malengo yako majuma haya machache ya mwisho, yaelekea umekuwa ukipata shauku ya kuwashirikisha wengine yale unayojifunza. Ufuasi kiasili huleta hisia ya furaha ya kutambua kusudi katika maisha ya mtu. Huamsha shauku ya kuwabariki wengine.
Lakini linapokuja suala la kuwafanya wanafunzi, wachache ndio wenye wazo halisi la kufanya. Naanzia wapi? Ni hatua gani zinazohusika? Inafanyaje kazi kweli? Wengine, wakiwa na shauku ya kuanza, wanazindua harakati kamili ya kubadilisha kanisa lao zima, na wanashangaa, labda kuvunjika moyo, kwa hali dhihiri ya ukosefu wa shauku. Wanajiuliza labda walikosa kitu fulani. Suluhisho katika hali zote mbili ni kufuata kile tunachokiita Mfumo wa Usahibu.
Mfumo wa Usahibu
Hatua ya kwanza katika kuanzisha kazi ya kuwafanya wanafunzi ni kuanza kutazama huku na huko. Wakristo wanaotuzunguka wanataabika katika maisha yao ya kiroho, na wengi wangekuwa tayari kufanya jitihada za kweli ikiwa wangekuwa na mtu wa kuwatia moyo, na kuwasaidia kupiga hatua fulani. Ili kuianza huduma yako ya kuwafanya wanafunzi, endelea kuwa macho tu katika kuwatafuta watu wanaoonesha shauku ya kukua katika maeneo mahususi ya uanafunzi. Eneo hilo la shauku linaweza kuwa yoyote miongoni mwa yafuatayo:
- Kukariri Maandiko. Labda mtu atakusikia ukinukuu aya fulani na kuelezea anavyotamani angekariri hivyo.
- Maombi. Mtu anaweza kueneza kuwa maisha yake ya maombi si madhubuti kama ambavyo angependa yawe. Au kwamba anatamani angekuwa na mtu fulani wa kusali naye.
- Kesha la Asubuhi. Idadi ya kushangaza ya waumini wana maisha maombi duni au hawana kabisa. Na hawajui hasa jinsi ya kujifunza.
- Matumizi Binafsi. Je, unamjua mtu anayehangaika ili kutekeleza Neno la Mungu maishani mwake, katika eneo fulani? Labda unaweza kumwunga mkono.
- Kushuhudia. Endapo unajihusisha katika aina fulani ya huduma, inawezekana kumpata rafiki anayetaka kujumuishwa mahali fulani.
Orodha hii haina mwisho, kwa kweli, lakini hudhihirisha wazo rahisi: watafute watu wenye nia ya kukua kiroho katika eneo fulani maalumu. Na utumie hilo kama mlango wazi wa kuanza kuwekeza maishani mwake.
Kukutana Pamoja
Mara tu unapompata mtu aliye na shauku ya kweli katika kipengele fulani cha uanafunzi, mwendee umweleze kuhusu kukutana pamoja ili kutiana moyo. Tunapendekeza mikutano ya kila juma, lakini kulingana na hali, ratiba zingine zinaweza kufanya kazi. Na mikutano hiyo si lazima iwe mirefu—uwe tu muda wa kutosha kuweka malengo machache, kueleza jinsi ulivyofanya katika malengo ya juma lililopita, na kusali pamoja. Si lazima hata iwe ana kwa ana: ratibu muda mahususi na kukutana kwa simu, au mawasiliano kwa video.
Epuka kugeuza mikutano hii kuwa tukio la darasa au mafunzo. Badala yake, unamtafuta tu “sahibu” wa kufanya kazi nawe katika kutimiza lengo fulani la kiroho la pamoja. Utapata fursa za kumshirikisha nyenzo mbele ya safari, lakini kama mshirika zaidi, kuliko mwalimu. Kwa kweli, mara nyingi hufanikiwa vizuri zaidi kuwatafuta watu wenye shauku ya kukua katika maeneo unayohisi kuwa wewe ni dhaifu. Kujua kwamba mtakutana kila juma na rafiki, na kuwajibika ili kutimiza malengo mliojiwekea pamoja kutakuhimiza kuwa mwaminifu zaidi. Na uwazi wako, matatizo, na azma yako binafsi, vyote vitathibitika kuwa uvuvio kwa mshirika wako!
Unaweza hata kukuza uhusiano na zaidi ya sahibu mmoja. Kutana na mmoja kwa ajili ya maombi, mwingine kufanyia kazi aya ya kukariri, na hata mwingine kwa ajili ya matumizi ya binafsi ya aya hizo, au aina fulani ya huduma. Sote tunabanwa na muda, lakini ikiwa tuna nia ya dhati ya kupanda juu zaidi katika kutembea kwetu pamoja na Mungu—jambo bora tunaloweza kufanya ni kumtafuta mtu anayetaka kukua katika eneo lolote tulilo dhaifu, na kujitahidi kufikia ubora pamoja!
Umuhimu wa Kujitoa
Tangu mwanzo, Mungu ametumia aina hizi za mahusiano kuwabadilisha waumini. Tunahitaji mausia haya na kutiwa moyo, ikiwa tunataka kuuepuka udanganyifu wa dhambi (Waebrania 3:13). Na itakuwa muhimu hata zaidi kadiri tunapoona kurudi kwa Kristo kukikaribia (Waebrania 10:24-25). Lakini mahusiano haya hufanikiwa yakijengwa tu kwenye mwenendo wa
kujitoa.
Mwombe Mungu akuongoze kwenda kwa wale watakaothibitika kujitoa kwa dhati, kisha uwe tayari
kujitoa kwao.
Vikosi vya Waumini
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 7 > Kielelezo
Gurudumu la Mwanafunzi Larejelewa