Ahadi za Mungu

Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 3 > Dokezo

     

Dokezo:


Mhariri hapa. Tunatazamia kuwasilisha zana nyingine kwa ajili ya uanafunzi bora. Hususan, tutaenda kuangalia kuhusu maombi. Watu wengi hufikiria sala kuwa jambo fulani la ajabu au fumbo—lakini ni muhimu sana, na kuna kanuni za msingi ambazo kila Mkristo anapaswa kuelewa. Je, unatamani kuwa hodari katika maombi? Somo la juma hili linaweza kusaidia!

Sala ndiyo njia ambayo kwayo tunapokea baraka zilizoahidiwa katika Neno la Mungu. Lakini mara nyingi sana tunapuuza muda wa maombi. Tunaahidi kuombea familia na marafiki, lakini kamwe hatujawahi kufikia hatua kukumbuka kufanya hivyo. Tunadai ahadi katika aya fulani ya Biblia na kisha tunakata tamaa kabla ya kupokea kile tunachoomba. Ufumbuzi ni upi? Wengi wamegundua kwamba ni shajara ya maombi.

Anzisha yako mwenyewe, na punde utaona maisha yako ya maombi yakiimarika zaidi. Utajikuta ukiomba kwa utaratibu zaidi na kwa ustahimilivu zaidi. Maombi yako yatakuwa mahususi zaidi, na yenye mfungamano wa karibu zaidi na Neno la Mungu. Na unaweza tu kuanza kuona majibu kuliko wakati wowote uliopita!

Mhariri,
Amefichwa katika Kristo

These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST

Ahadi za Mungu

Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 3 > Malengo


Jina:                                                     Saini:                                         
Tarehe:                                         


Kamilisha Uchunguzi wa Biblia unaoitwa Ahadi za Mungu. Kuweza kudai ahadi ambazo umezihifadhi moyoni mwako ni manufaa mojawapo muhimu ya kukariri Maandiko. Unaposoma somo lililo mbele yako, hakikisha unalifikiria kama muda wa ushirika wa faragha kati yako na Bwana.

Aya yako ya kukariri inayofuata ni nzuri: Warumi 4:20. Hakikisha unatafakari aya hizi unapojifunza. Fikiria hasa inachosema kuhusu dhima ya Maandiko katika sala. Pia, endelea kurudia aya zingine ulizojifunza hadi sasa angalau mara moja kila siku.

Soma Mapendekezo ya Kutendea Kazi mwishoni mwa kijitabu hiki kuhusu jinsi ya kuanzisha shajara ya maombi. Kisha, tumia muda fulani juma hili kuandika mahitaji machache ya maombi na kuyapanga katika shajara yako ya maombi. Hakikisha unafuata mapendekezo kwa uangalifu. Tabia ya kutumia mara kwa mara shajara ya maombi inaweza kufanya mengi katika kuimarisha imani yako.

Katika juma hili fanya kazi ya kujifunza kielelezo cha Upinde wa Ahadi Endelea kupitia upya vielelezo vyote ambavyo tumevibainisha hadi sasa. Kama inasaidia, viandike kwenye kadi ndogo, na uyapitie upya pamoja na aya zako unapofanya marudio yako ya kila siku. Utazijua muda si mrefu!


Maombi ni ufunguo katika mkono wa imani
Ambao hufungua hazina za mbinguni


Ahadi za Mungu

Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 3 > Uchunguzi wa Biblia

Nanyi mkiomba lolote kwa jina Langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Yohana 14:13


1.

Yesu anafanya nini katika kila moja ya aya zifuatazo?

Mathayo 14:23


Marko 1:35


Luka 5:16


Luka 6:12



2.

Yesu alisema tunapaswa kuombaje, na kwa nini? Mathayo 6:6




3.

Ni somo gani kuhusu maombi alilofundisha Yesu katika mifano ifuatayo?

Luka 11:1-8




Luka 18:1-8

4.

Ni vikwazo gani vitatu vinaweza kuzuia ombi lisijibiwe?

Yakobo 1:6-7




Yakobo 4:3




Zaburi 66:18




5.

Ni ahadi gani wanazopewa wale wanaoshinda vikwazo hivi?

Marko 11:24




I Yohana 5:14-15




I Yohana 3:21-22





Kumbuka: Kukariri Maandiko mara nyingi huwa na matokeo yenye nguvu katika maombi kwa kuwa husaidia kushinda vikwazo vyote vitatu dhidi ya maombi fanisi: kukosa imani (Warumi 10:17), maombi potofu (Isaya 30:21), na dhambi inayoendekezwa (Zaburi 119:11).

6.

Ni yapi baadhi ya mambo tunayopaswa kuyaombea?

Wagalatia 5:22-23


Wafilipi 4:19


Isaya 48:17


Waefeso 6:19


Wafilipi 1:3-6


Mathayo 9:37-38



7.

Kwa nini maombi yana nguvu sana? Waefeso 3:20




Nini kusudi lake kuu? Waefeso 3:21




8.

Je, uko tayari kiasi gani kujitoa sasa hivi ili kutenga muda kwa ajili ya maombi ya muda mahususi, yenye utaratibu? Kwa nini usiandike jibu lako liwe sala fupi kwa Mungu?

Ahadi za Mungu

Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 3 > Mapendekezo ya Kutendea Kazi

Wanafunzi waaminifu daima wametambua umuhimu wa sala. Walisoma ahadi adhimu katika Biblia walizopewa wale wanaosali. Wanasikia visa vya maisha ya maombi yenye bidii ya wanaume na wanawake wakuu waliompenda Mungu—na majibu ya kustaajabisha waliyopokea. Wanamwona Yesu Mwenyewe, akitumia usiku kucha katika maombi ya bidii. Na ndani kabisa, wao pia, wanatamani sana kuwa hodari katika maombi.

Wengi wamegundua shajara ya maombi binafsi kuwa kile hasa kilichohitajika ili kujenga maisha ya maombi thabiti zaidi. Anzisha yako mwenyewe, na punde utajikuta unakuwa imara zaidi katika maombi. Na unaweza kugundua kitu kingine zaidi—kwamba kusudi halisi la maombi ni badiliko la mioyo yetu wenyewe! Ni zaidi ya kuomba vitu tu, hutusaidia kumfuata Yeye.

Kuanzisha Shajara ya Maombi

Ili kugeuza daftari lako la Kesha la Asubuhi kuwa shajara ya maombi, tenga sehemu moja kwa ajili ya mambo ya kuombea. (Au ukipenda, ziweke kwenye daftari la pili). Kila jambo la kuombea linapaswa kuandikwa kwenye karatasi tofauti—na hujumuisha mambo yafuatayo kwenye kila ukurasa:


Kutumia Shajara Yako ya Maombi

Mara tu unapokuwa umeandika idadi kadhaa ya karatasi za mahitaji ya maombi, anza kuyaombea kwa vipindi maalumu—kama sehemu ya muda wako wa Kesha la Asubuhi. Iwapo huna muda wa kutosha wa kuombea kila hitaji, weka alama mahali unapoishia na uanzie hapo kesho yake. Anza tena mwanzoni unapofika mwisho.

Ikiwa una mahitaji mengi, tunapendekeza uyatenge katika sehemu mbili tofauti: sehemu ya kipaumbele kwa ajili ya mahitaji unayotaka kuombea kila siku, na sehemu nyingine ya mahitaji ya kawaida unayoweza kuyaombea taratibu, machache kila siku. Iwapo Roho akikugusa kuombea mahitaji fulani—usisite kufanya hivyo, hata kama itamaanisha kwenda kinyume na utaratibu. Shajara yako ya maombi imekusudiwa kukusaidia, siyo kukuwekea vikwazo. Inaweza kufuata utaratibu na kubadilika kwa wakati mmoja.

Endelea kuombea mahitaji maadamu yako katika shajara yako ya maombi. Maombi mengi hujibiwa kidogo kidogo—kwa hiyo andika kwa uaminifu ushahidi wowote kwamba Mungu yuko kazini. Wakati mwingine, unaweza kuhisi kuongozwa kurekebisha hitaji fulani, kadiri ambavyo uelewa wako wa mapenzi ya Mungu unakuwa dhahiri zaidi. Au labda hata kuacha kabisa mojawapo. Andika tu sababu zako, na ufanye mabadiliko hayo. Lakini kwa mahitaji yale yanayopatana na Maandiko kikamilifu, dumu kuwa thabiti katika maombi. Mungu atalijibu Neno Lake! Hifadhi mahali fulani maombi yaliyojibiwa, kama chanzo cha imani na uvuvio kwa siku zijazo.

Kuunda shajara ya maombi ambayo ni madhubuti na inayobadilika daima kama hii, ni tofauti sana na kile kinachofundishwa kwa kawaida. Ili kukusaidia kuelewa zaidi jinsi inavyofanya kazi, tumetayarisha kozi nzima fupi kuhusu hili inayoitwa Siri za Maombi. Unaweza kujiandikisha kwenye WWW.FAST.ST/SECRETS. Pia tuna sampuli ya karatasi ya hitaji la maombi ili kuonesha jinsi hii inavyoonekana, fomu tupu unazoweza kuchapa na kutumia kwa ajili ya shajara yako ya maombi, na hata Shajara ya Maombi mtandaoni. Ziangalie kwenye WWW.FAST.ST/BT-GIFT.

Kidokezo cha Kukariri Maandiko: Njia bora ya kuimarisha maisha yako ya maombi ni kukariri ahadi mahususi zinazohusiana na mahitaji yako ya maombi muhimu zaidi. Kuna kitu fulani madhubuti juu ya kudai ahadi za Mungu katika maneno halisi ya Maandiko. Ijaribu!

Azma Muhimu

Ili kuishi maisha ya uanafunzi, tunategemea kikamilifu nguvu za Mungu. Bila Kristo, hatuwezi kufanya lolote. Na kadiri maisha yetu yanavyozidi kuwa yenye shughuli nyingi, ndivyo hitaji letu la maombi linavyoongezeka zaidi! Kwa hiyo maombi ni kukiri kwamba tunamtegemea Mungu—na ukosefu wa maombi ni uthibitisho wa kujitosheleza nafsi. Unapotafakari maisha yako mwenyewe, kwa nini usifikirie kuweka azma ya dhati ya kutenga muda katika maombi? Itakupatia nguvu kwa ajili ya kila kipengele kingine cha mwenendo wako wa Kikristo.

Ahadi za Mungu

Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 3 > Kielelezo

Upinde wa Ahadi