Kesha la Asubuhi
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 2 > Dokezo
 |
|
Dokezo:
Habari! Mhariri tena. Karibu tena kwenye somo lingine la kusisimua! Somo hili linaangalia moja ya mada muhimu zaidi katika programu nzima. Kwa hivyo tumia muda mwingi katika maombi unaposhughulikia maswali. Mambo haya ndiyo kiini cha maana ya kumfuata Kristo!
Wakristo mara nyingi huambiwa wanapaswa kuichunguza Biblia kila siku, na ni kweli. Lakini ni wangapi ambao wamewahi kuketi na mtu fulani halafu akawaonesha jinsi ya kujifunza Biblia kwa njia ambayo wanaweza kupata jambo fulani kutoka kwayo? Ni wangapi wanafundishwa jinsi ya kuyatafakari Maandiko—au jinsi ya kuyatumia maishani mwao. Naam, hivyo ndivyo hasa utakavyojifunza katika somo la juma hili!
Watu wengi wanataka muda wa kina wa kuichunguza Biblia kila asubuhi, lakini hawajui jinsi gani. Jifunze kijitabu hiki kwa makini, na utagundua dondoo za kuufanya wakati wako pamoja na Mungu uwe hai. Itahitaji juhudi fulani—lakini shikamana nayo. Na fanya katika kiwango chako bora. Habari njema ni kwamba Mungu anasubiri kukutana nawe.
Mhariri,
Amefichwa katika Kristo |
These resources are licensed for personal study by . Please do not distribute.
Copyright © 2026, FAST Missions, All rights reserved. WWW.FAST.ST
Kesha la Asubuhi
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 2 > Malengo
 |
Kamilisha Uchunguzi wa Biblia unaoitwa Kesha la Asubuhi. Kutumia muda maalumu katika Neno la Mungu kila siku itakupatia mwongozo thabiti, faraja na ufahamu endelevu. Pamoja na aya nyingi mpya za kuhifadhi moyoni mwako! Unapojifunza, kumbuka kumwomba Mungu ufahamu maalumu. |
 |
Aya yako ya kukariri juma hili ni Zaburi 143:8. Hakikisha unakariri aya hii kwa usahihi na kisha uirudie pamoja na aya uliyojifunza juma lililopita—angalau mara moja kila siku. Tutajadili umuhimu wa mapitio ya kila siku katika somo la baadaye. |
 |
Soma Mapendekezo ya Kutendea Kazi kuhusu jinsi ya kujifunza Biblia. Hakikisha unaelewa namna ya kutofautisha kati ya kanuni na mradi. Kuanzisha muda thabiti wa Kesha la Asubuhi, uliojaa tafakari na matumizi, ni msingi wa uanafunzi. |
 |
Fanyia kazi kielelezo chako kinachofuata, Baiskeli ya Kesha la Asubuhi, na utafakari masomo yanayofundishwa hapo, kadiri unapofanyia kazi somo la juma hili. Kujifunza vielelezo hivi kutasaidia kudumisha akilini mwako maarifa unayopata. Kadhalika, hukupatia kitu fulani cha kuwashirikisha wengine! Endelea kufanyia marudio kielelezo cha juma lililopita, vilevile—hadi uweze kuvikumbuka vyote viwili kikamilifu. |
Kutumia muda katika Neno la Mungu
Hufumbua macho yako ili yatazame mambo yasiyoonekana
Kesha la Asubuhi
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 2 > Uchunguzi wa Biblia
Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome; hakuna hata mmoja katika hao wote atakayekosa kuwepo. Isaya 34:16
1. |
Hivi Mtunzi wa Zaburi anaelezeaje shauku tunayopaswa kuwa nayo kwa ajili ya Mungu katika kila moja ya aya zifuatazo?
Zaburi 42:1-2
Zaburi 63:1
Zaburi 84:2
|
2. |
Ni njia gani moja makini tunayoweza kutosheleza shauku hii ya maarifa ya Mungu?
Kumbukumbu la Torati 17:19
Matendo 17:11
Kumbuka: Hakuna chochote kinachoweza kuuridhisha moyo wa mwanadamu kama mwenendo wa kumtazama Kristo kila siku kupitia mazoea binafsi ya kujifunza Maandiko. |
3. |
Ni wakati gani unaofaa zaidi kukutana na Mungu kwa ajili ya utaratibu binafsi ya kujifunza Biblia? Mithali 8:17
Kumbuka: Mungu anawaahidi baraka maalumu wale wanaomtafuta mapema: yaani, kwamba watampata!
|
4. |
Nini kinachopaswa kuunganishwa na kujifunza ili kuyafanya Maandiko yawe na manufaa?
Yoshua 1:8
Zaburi 1:2-3
I Timotheo 4:15
|
5. |
Ni lipi kusudi kuu la kutafakari?
Zaburi 119:59-60
I Wathesalonike 4:1
Kumbuka: Linapokuja suala la kuwa mfuasi wa Yesu Kristo, matumizi binafsi ya maandiko ndicho kiini hasa cha mambo yote. |
6. |
Tunapaswa kufanyaje ujuzi maalumu ambao Mungu anatupatia kupitia Neno? Kumbukumbu la Torati 6:6
Je, tunahatarisha nini ikiwa hatufanyi hivyo? Yakobo 1:22-25
Je, matokeo yatakuwa yapi tukifanya hivyo? Zaburi 40:8
|
7. |
Nini kitakachotokea hatimaye kadiri tunapojifunza kuichunguza Biblia yetu kwa ufanisi, siku baada ya siku? II Wakorintho 3:18
|
8. |
Je, uko tayari kujitoa sasa hivi kuanzisha muda mahususi kwa ajili ya hatua binafsi ya kuichunguza Biblia kila asubuhi? Kwa nini usiandike jibu lako liwe sala fupi kwa Mungu? |
Kesha la Asubuhi
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 2 > Mapendekezo ya Kutendea Kazi
Pengine hakuna kitu muhimu zaidi kwa mwanafunzi wa Yesu Kristo kuliko kutumia muda peke yake pamoja Naye mwanzoni mwa kila siku, kupitia Neno. Ili kumfuata Kristo kwa dhati, lazima tuwekeze muda wa kuyachunguza Maandiko, kutafuta ufahamu binafsi katika maisha, na kumsikiliza Bwana aseme na mioyo yetu. Ushirika halisi, thabiti pamoja na Mwokozi ndicho kiini cha uanafunzi wa Kikristo. Tunauita muda huu
Kesha la Asubuhi. Ibara hapa chini zinapendekeza dondoo chache rahisi za kunufaika vilivyo katika wakati wako pamoja na Mungu.
Mpango wa Kujifunza Kila Siku
Anza kwa kutafuta daftari maalum lenye kurasa zisizoshikamana kwa ajili tu ya Kesha lako la Asubuhi. Hakikisha lina karatasi za kutosha na uwe na penseli au kalamu na Biblia karibu. Kupangilia daftari lako itakusaidia kuepuka kupoteza muda kujaribu kutafuta mambo yalipo. Kwa ajili ya muda wako halisi wa kusoma, mfumo huu rahisi wa hatua nne utakusaidia kujikita kwenye mabadiliko ya maisha:
- Jitayarishe. Kabla hujaanza kulichunguza Neno, tumia muda fulani katika maombi, ukimwomba Mungu akufundishe kupitia Roho Wake. Ni Roho Mtakatifu pekee ndiye anaweza kulifanya Neno liwe hai. Tazama Yohana 14:26, Yohana 16:13. Unapoomba, wasilisha kwa Bwana mahitaji, matatizo, maswali, mipango maalumu, n.k., na umwombe azungumze nawe kuhusu maeneo hayo.
- Fafanua. Fungua ukurasa mpya na uandike tarehe na kifungu utakachokuwa ukijifunza. Fanyia kazi kile kiasi tu kadiri unavyopata muda wa kutafakari vizuri—hata kama ni aya 6-8 tu. Soma kifungu hicho kizima mara kadhaa hadi uanze kufahamu kile ambacho mwandishi anasema. Kisha, andika maelezo mafupi ya kifungu hicho kwa maneno yako mwenyewe. Mara nyingi ni vyema kusoma kitabu kizima cha Biblia kimoja kwa wakati, kila asubuhi ukianzia ulipoishia siku iliyopita. Tunapendekeza kuanza na vitabu vifupi vya kivitendo kwanza, kama vile Yakobo au I Wathesalonike, ili kukusaidia kujizoeza aina hii ya kujifunza.
- Kanuni. Kisha, tumia muda fulani kutafakari kifungu husika. Tafuta kanuni—maagizo ya maadili yanayoongoza jinsi ulimwengu wetu unavyofanya kazi. Mara nyingi njia rahisi zaidi ya kupata kanuni ni kujiuliza maswali: Je, kuna dhambi fulani ya kuepuka? Je, kuna sifa nzuri ya kitabia ili kuikuza? Je, kuna uhusiano fulani wa chanzo-matokeo ambao umedhihirishwa katika kifungu hiki? Je, kuna dhihirisho la mapenzi ya Mungu? Ahadi? Shughuli mbaya ya kuacha? nk. Kwa mazoezi kidogo punde utajikuta unaweza kwa asili kuuliza maswali sahihi kabisa. Kanuni zitaonekana kuibuka kwenye ukurasa. Mara tu ukiona mojawapo, iandike kwenye karatasi yako.
- Miradi. Kuipata kanuni ni nusu tu ya vita. Lazima uendelee baada ya hapo kuitumia kwa ajili ya maisha yako ya binafsi. Hii inamaanisha kuibadili kanuni hiyo kuwa mradi fulani kwa kuuliza hata maswali mengine zaidi, kama vile: Nani? Nini? Lini? Wapi? na Jinsi gani? Lipi hasa ambalo aya hiyo inapendekeza ulifanye? Kadiri Roho Mtakatifu anapoleta miradi fulani akilini, iandike, ukiikagua ili kuhakikisha hukidhi kigezo cha KIBIMA (Kimaandiko, inafanyika, binafsi, na mahususi). Kisha, azimu kutekeleza matumizi yako mara moja. Endelea kutafuta kanuni na miradi maadamu una muda wa kusoma.
Kujifunza kugundua kanuni kutoka kwenye kifungu fulani, na kisha kuzibadili kuwa miradi siyo rahisi kila wakati. Ili kukusaidia kumudu ujuzi huu, tumetayarisha kozi nzima fupi kuhusu hili, yenye kichwa cha habari kisemacho
Warsha ya Matumizi. Unaweza kujiandikisha kwenye
WWW.FAST.ST/AWE. Pia tuna sampuli za vidokezo vya kesha la asubuhi ili kueleza jinsi ambavyo somo husika linaweza kuonekana, fomu tupu unazoweza kuchapa na kutumia kwa usomaji wako binafsi, na zana mbalimbali za kujifunza Biblia mtandaoni. Ziangalie kwenye
WWW.FAST.ST/BT-GIFT.
Kidokezo cha Kukariri Maandiko: Unaposoma vitabu mbalimbali vya Biblia, utagundua aya nyingi ambazo utataka kukariri. Andika marejeleo haya kwenye kipande cha karatasi na uweke orodha katika daftari lako la Kesha la Asubuhi. Punde utakuwa na aya nyingi bora unazoweza kuchukua muda mwingine unapotafuta aya ya kujifunza!
Umuhimu wa Kujitoa
Dondoo muhimu zaidi ya kudumisha Kesha la Asubuhi ni kujitoa—maana bila hiyo, hauwezi kuwepo mwendelezo thabiti. Kesha la Asubuhi lazima liwe sehemu ya maisha yetu kila siku, hata iwe kwa muda mchache tu kila asubuhi. Weka lengo la kujenga tabia yenye nguvu kiasi cha kudumu maisha yako yote.
Azimu. Usikate tamaa. Fanya mabadiliko yoyote yanayohitajika kwenye ratiba yako ili kupata muda bora pamoja na Bwana—kila siku! Ni muhimu.
Kesha la Asubuhi
Kozi Mafunzo ya Msingi > Juma la 2 > Kielelezo
Baiskeli ya Kesha la Asubuhi